Jumamosi nyingine kwa upendo wa Mungu tunaweza kukutana tena kwa ajili ya kujadiliana kuhusu changamoto mbalimbali maisha na mapenzi. Somo la leo linahusu kujitesa kwa muda ili uweze kufanikiwa katika kutimiza malengo au ndoto zako.
Ndugu yangu mtu yeyote unayemuona au kumsikia kuwa kafanikwa basi ni lazima atakuwa alijitesa kama siyo yeye basi kuna watu waliteseka kwa ajili yake.Huwezi kufanikiwa kwa hisia, fikra, maneno au kwa kusubiri f’lani akulete au ushushiwe mafanikio unayoyataka.
Si rahisi kufanikiwa kwa kuwa msikini wa kufikiri au mtu ambaye unapenda kuwa tegemezi.Mafanikio yoyote yanahitaji uteseke, ujitume, uthubutu ili kuweza kuyapata au kuyafikia.
Ukitaka kufanikiwa katika jambo fulani ni lazima ukubali kuteseka kwa malengo, kwa mfano unaishi na mtu lakini inaonekana anakunyanyasa basi ni lazima uvumilie yale mateso wakati unatafuta namna ya kuanza kujitegemea, lazima uumize kichwa ni kwa namna gani utaweza kupata kazi ya kukuingizia kipato kitakachokuwezesha kujikimu kwa kulipa kodi, chakula ma mambo mengine.
MATESO YA KUJIAJIRI
Hapa nitajaribu kuzungumza na mtu ambaye anatamani atoke kimaisha lakini anashindwa, yumkini umeajiriwa lakini unaona kabisa una kila sababu ya kujiajiri ila unashindwa, basi lazima uendele kufanya kazi kwa mateso ya mafanikio, endelea kuumia na kuteseka kwa malengo.
Malengo yako unaweza kuweka ya mwezi mmoja, miezi mitatu, na kuendelea inategemea na ndoto zako. Kwa hiyo unaweza kuchagua mwenyewe uteseka kwa muda gani na kwa ajili ya kupata nini? Unachotakiwa ni wewe kuwa na uchungu na kile ambacho unataka kukifanya au kukikamilisha.
MATESO MENGINE NI YA MATUMIZI
Kama ulikuwa unatumia Sh.10,000 kwa siku basi punguza anza kutumia 5,000. Kama asubuhi pekee, ulikuwa unakunywa chai ya Sh. 3,000 basi anza kunywa ya 1,500 kwa maana ya kwamba kama ulikuwa unakunywa chain a chapatti 2 au zaidi basi kunywa chai na chapati moja, utumbo utapwaya lakini huwezi kufa kwa kutokula chapati mbili.
Tena chai hiyo unaweza kuivutia muda kidogo angalau saa nne au saa tano ndipo ukanywa ili ikusaidie kukufikisha kwenye chakula cha mchana.
Ukishapiga chai na chapati yako moja amchain a kitafunwa kimoja kisha ukasubiri mchana ndiyo ukala kwa kushiba au unaweza kuipotezea kabisa chai kwa muda wa miezi 3 ili kuangalia kama malengo yako yamefanikiwa. Kuwa na malengo yasiyo kufikirisha na kukuumiza kiakili, kimwili na kimtazamo, hakikisha unajiwekea malengo yenye maumivu ili uweze kufanikiwa lasivyo utaendelea kuwa hivyohivyo siku zote.
Kwa ushauri wa mahusiano, mada za mahaba, hadithi, machombezo, mikasa ya kweli ya mapenzi na ujasiriamali. Jiunge na Mi&u SMS au Mi&u WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
#Mi&u