Idadi ya tuliowengi bila ya
kujali ni maskini au tajiri tumezaliwa
katika familia maskini. Hata unapoona wengine wanakuwa wamefanikiwa sana, hiyo
haina maana kwamba wao wametakotea katika koo au familia za kifalme, bali ni
matokeo ya nguvu na juhudi zao wenyewe.
Kwa mantiki
hiyo inamaanisha hivi, ili uweze kupata utajiri, mbali na juhudi binafsi zipo
sheria ambazo mtu anatakiwa azifuate ili kufikia lengo hilo. Na kwa kufuata
sheria hizo haitajalisha wewe umetokea katika familia gani au umetokea katika nchi
au wewe ni wa rangi ipi ni lazima utafanikiwa.
Kwa kusoma
makala haya ya leo, utajifunza sheria chache za msingi ambazo mtu unatakiwa uwe
nazo au uzifahamu ili zikusaidie kujenga utajiri hata kama umetokea familia
maskini. Uwezo wa kufikia utajiri unao tena sana, ni suala la kuamua na kuanza
kutekeleza sheria za mafanikio. Sheria hizo ni zipi? Twende pamoja katika somo.
1.
Tengeneza tabia za kukuwezesha kuwa tajiri.
Utajiri
haujengwi kwa bahati mbaya hata kidogo. Zipo tabia ambazo unatakiwa uzijenge
ili zikusaidie kutengeza msingi imara wa utajiri unaotaka kwenye maisha yako. Tabia
ya kujiwekea akiba, kutunza muda na kujenga
maamuzi sahihi ya kimafanikio ni moja ya tabia bora ambazo ukiziendeleza kwa
muda zinakupa mafanikio ya wazi.
Angalia
sana katika maisha yako usije ukajuta kwa sababu ya tabia zako mbaya ambazo
zitakuangusha na kukufanya ukashindwa kufikia
utajiri. Kuwa makini na tabia hizo, jikague na jenga tabia za kukuwezesha
kufanikiwa. Kwa kadri unavyojenga tabia hizi kila siku, ndivyo utazidi
kukaribia mafanikio yako kwa sehemu kubwa.
2. Fanya kazi kwa juhudi sana.
Ikiwa
ndio unaanzia chini kabisa huna kitu, hakuna kitakachoweza kukutoa hapo ulipo
zaidi ya kufanya kazi kwa juhudi sana. Hapa inabidi ufanye kazi kwa bidii tena
huku ukiwa na nidhamu ya hali ya juu kwa kuhakikisha kila ukipatacho unakitunza
vyema na kinakusaidia kufanikiwa kwako.
Kama
umeamua kujitoa kisawasawa na kufanya kazi kweli na kuachana na maneno,
utafanikiwa. Hii ni sheria inayotumiwa na watu karibu wote wenye mafanikio
makubwa duniani. Siku zote watu hao ni wa kufanya kazi kwa bidii kubwa hali inayopelekea
kuleta mafanikio yao ya uhakika na kujenga utajiri.
3. Tengeneza vyanzo vingi vya fedha.
Hakuna
utajiri unaojengwa kwa kutegemea chanzo kimoja cha pesa, utajiri unajengwa kwa
kujiwekea vyanzo vingi vya pesa. Kama una chanzo kimoja cha pesa na una nia ya
kuwa tajiri hauataweza kuwa hivyo. Siri au sheria ya kuwa tajiri inakutaka wewe
kutengeneza vyanzo vingi vya pesa.
Vyanzo
hivyo vya pesa vitaingiza pesa bila kujali sana wewe unafanya kazi moja kwa
moja au haufanyi. Matajiri wengi ndivyo wanavyotengeneza utajiri wao na hii ni siri
mojawapo ambayo unatakiwa uijue kwa ufasaha. Huhitaji sasa kusita sita , weka
vyanzo vingi vya pesa utengeneze utajiri wako.
4. Tambua namna ya kutunza pesa zako.
Itakuwa
ni kazi bure kama unatafuta pesa, hujui
namna ya kuzitunza vizuri. Kuna watu ambao tatizo sio namna ya kupata pesa,
bali ni jinsi ya kuzitunza pesa hizo. Utakuta mtu anapata pesa kweli, lakini
matumizi yake yapo juu sana, hicho ni kitu ambacho ni sumu au kiziuzi cha
mafanikio yake moja kwa moja.
Inabidi
ufike mahali uwe na nidhamu ya hali ya juu, juu ya pesa zako, achana na
matumizi ya hovyo, hayawezi kukufikisha popote. Kila wakati kaa chini na elewa
namna ya kujifunza juu ya kutumia pesa zako kwa busara. Pesa zako zisije
zikakufanya ukawa kama mwendawazimu, tulia ili ujenge utajiri wako.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.Mi&u
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.