Sunday, January 31, 2016

Published 1/31/2016 07:06:00 PM by with 0 comment

NATAMANI HATA KUJIUA!


Mimi ni msichana wa miaka 20, nilijichanganya kwa kuanza mapenzi nikiwa bado sijakomaa kifkra, nilipata mpenzi ambaye alinipa ujauzito ila baada ya ujauzito huo alichonitenda.... sitosahau kwani alinitelekeza na kunifanya niishi maisha ya shida kwani nyumbani nilifukuzwa baada ya kuacha shule  kwa sababu ya ujauzito wake.
Ni miezi 4 sasa siko naye maisha yangu ni duni hapa nilipo nimehifadhiwa kwa msamaria mwema. sina kazi, mlo wa siku ni shida, natamani hata kujiua, naomba msaada wako wa hali na mali au unanishauli nifanyaje?


Read More
      edit

Saturday, January 30, 2016

Published 1/30/2016 06:52:00 AM by with 0 comment

MAPENZI YANAVYOTESA!


Mimi ni Binti nina mika kadhaa, nina mika 2 tangu nimeachana na mpenzi wangu ila kiukweli toka moyoni mwangu jamaa bado nampenda nimejitahidi kumsahau nimeshindwa, nifanyeje wadau?
Read More
      edit
Published 1/30/2016 06:37:00 AM by with 0 comment

MAMBO YANAYOFURAHISHA FARAGHA-1


ASANTE Mwenyezi Mungu kwa kuiona siku ya leo, tunakutana tena katika kilinge chetu hiki kama ilivyo ada, bado tunaendelea kujifunza namna mbalimbali ya kufanya tunapokuwa faragha na wenza wetu. Kwa kifupi mada hii ya faragha imewavutia wengi sana ambao wameomba niendelee kuifafanua zaidi.


Nianze kwa kusema kila kitu kinahitaji hamasa au hisia ili kiweze kufanyika katika hali nzuri, ndivyo hivyo hata mapenzi nayo yanahitaji hamasa ili kuweza kuamsha hisia za mwenza wako na hatimaye kukutana faragha. Mnapokuwa faragha kuna kipindi inabidi mpongezane kwa kazi nzuri mliyoifanya ya kuhakikisha kila mtu anafurahia faragha yenu.

Leo nitazungumza kuhusu umuhimu wa vitu mbalimbali vinavyoweza kuifanya faragha yenu kuonekana ni nzuri na bora zaidi. Kuna vitu vingi ambavyo vinapaswa kufanyika ili kukamilisha faragha yenu kuwa yenye tija, baadhi yake ni kama ifuatavyo;

SAUTI YA KUBEMBELEZA

Ikumbukwe kwamba sauti ya mtu akiwa anazungumza wakati mihemko au mizuka haijampanda huwa ni sauti ya kawaida na inapotokea mihemko imepanda basi hubadilika, hiyo inayobadilika ndiyo ninayoizungumzia.

Kuna sauti f’lani za mahaba ambazo husikika watu wanapokuwa wamezama zaidi kwenye dimbwi zito la mahaba. Mfano; baadhi ya wanawake wamejaliwa kuwa na sauti f’lani za furaha au raha na zenye kuhamasisha wanapokuwa faragha na wenza wao, kiukweli sauti hizo zinastahili kuwepo ili kumhamasisha mwenza wako.

Sauti hizo za mahaba siyo tu kwa wanawake, hata kwa wanaume pia.
Kusikika kwa sauti hizo za mahaba hata kama mwenza wako atakuwa amechoka pindi anapozisikia au kuzifikiria sauti zile akilini mwake basi anapata nguvu mpya ya kuingia tena ulingoni.


Japokuwa kila mwanadamu ameumbwa na aina yake ya hamasa anapokuwa faragha, kwa hiyo kama hatakuwa na sauti za mahaba, basi anaweza kuwa na kitu kingine zaidi.

Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook na WhatsApp kujua mengi kuhusu mapenzi.
Mada hii itaendelea wiki ijayo.



MAMBO YANAYOFURAHISHA FARAGA-2

Watanzania tunu yetu kubwa tuliyojaliwa na Mungu ni amani, amani ndiyo imenifanya leo uweze kusoma mada hii ya mambo yanayofaa faraghaWiki iliyopita tulizungumzia kipengele kimoja cha sauti za kubembeleza leo nitaendelea na mambo mengine mazuri mnapokuwa faragha;

BUSU
Kama ulikuwa hujui busu ni zuri mnapokuwa faragha kwani linahamasisha sana kinyang’anyiro chenu, wakati mwingine ukipiga busu lililozuri linaweza kuwa ni kumbukumbu kwa mwenza wako kwa muda mrefu.

DEKO
Kudeka hasa unapokuwa faragha ni poa sana kwani inaonesha ni namna gani unajisikia furaha, amani, upendo kuwa na mtu ambaye ukimdekea anakufariji na kukubembeleza, ni nzuri hii kwa uhusiano, haijalishi cheo chako, umri au uwezo ulionao.



MINONG’ONO
Sauti za mahaba huwa ni zile za kunong’onezana zenye kujaa matamshi ya kubembelezana, minong’ono hiyo huhamasisha sana mnapokuwa faragha hasa baada ya kumaliza ngwe ya kwanza na kuitafuta ya pili.

Pongezi
Wengi hujisahau sana kutoa pongezi kwa wapenzi wao mara baada ya kumaliza tendo husika na matokeo yake wanakuwa kama vile wana ugomvi, mkimaliza kazi mwambie mpenzi wako, baby pole kwa kazi nzito uliyofanya.


FURAHIA
Pongezi pekee hazitoshi kama unahisi umefurahia huduma yake , mwambie kabisa ili na yeye ajue amefanya kazi nzuri aliyopaswa kufanya na hata kama hajafanya vizuri mwambie ukweli ‘ ila mai kwa leo mimi sijainjoi wangu, haikuwa kama siku ile…’’


VALISHANENI
Kama mliweza kushirikiana mwanzoni mwa zoezi kwa kusaidiana kutoa sehemu ya nguo zenu, vivyo hivyo mnapaswa kushirikiana pia katika kuvalishana mara baada ya kumaliza zoezi lenu.
Kimsingi mapenzi ni uwezo binafsi lakini pia ni suala la utundu na ujanja wa mtu katika kuhakikisha anaweza kumfikisha mwenza wake mahali anapohitaji kufika kwa maana ya kufikia kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Mpenzi msomaji usikose mada nyingine tamu wiki ijayo, pia usikose kufuatilia ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook na WhatsApp kujua mengi kuhusu mapenzi.

Na Gabriel Ng’osha-GPL

Read More
      edit

Friday, January 29, 2016

Published 1/29/2016 10:25:00 PM by with 0 comment

HIVI MAPENZI YAMEKUFANYIA NINI?


Mpenzi msomaji wa safu hii M&U shukrani nyingi zikufikie kwa maoni na ushauri wako. Baada ya wiki iliyopita kukupa mbinu za kupigania penzi lako kwa maana ya kulia au kulisusa siyo dawa, wiki hii napenda nijue wewe msomaji wa makala hii. Mapenzi yamekufanyia nini?


Ninaamini kila mtu atakuwa na jibu kulingana na vile mapenzi yalivyomfanyia katika maisha yake ya uhusiano.
Kwa kuanza tu, wapo watu waliofika ughaibuni kwa sababu ya kuwa na wenza wa nchi husika na mwenza wake kumkaribisha au kuamua kuishi naye katika nchi hiyo.

Wapo walioumia kiasi cha kutotaka kusikia tena kitu kinachoitwa mapenzi wala mpenzi, wengine wameshindwa kuendelea na masomo baada ya kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi wakiwa na umri mdogo, jambo lililowasababishia kushindwa kumudu vitu viwili kwa wakati mmoja.


Wapo waliofanikiwa kupata watoto wazuri na wenye kuwasaidia katika maisha yao, lakini pia wapo waliopata watoto watukutu walioshindikana na wazazi wao, wanasubiri tu waadhibiwe au wafundishwe na ulimwengu.
Wengine wamepata mafanikio baada ya kupata watoto werevu ambao wanawasaidia katika maisha yao ya kila siku.
 
Wapo wengine walioambulia kupata magonjwa ya ziana na sugu kwa sababu ya mapenzi bila kusahau kuna wengine walipotea kwenye ramani ya dunia, kisa kikiwa ni mapenzi.
Bila kusahau wapo waliofungwa jela kwa kubaka, kuuwa au tukio lolote lililosababishwa na mapenzi.

Kwa jumla mapenzi yamesababisha mambo mengi sana kwenye jamii inayotuzunguka, cha msingi ni kujiuliza, je, mapenzi unataka yakufanyie nini? Yakuambukize magonjwa ya zinaa kisha yakuue, yakuning’inize, yakutese na kukuteketeza au yakupatie watoto na familia bora ili ufurahie maisha. 

Au yasababishe kuongezeka kwa watoto wa mitaani na wanaoishi katika mazingira magumu? Au yakugombanishe kazini na bosi wako, mke au mume wa bosi wako?
Au yakutenganishe na ndugu zako au uvuruge maisha yako kwa kupigwa au kumpa mimba mwanafunzi mwenzio? Unataka mapenzi yakufanyie nini? Tafakari!
Usikose wiki ijayo kwa mada nyingine. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Facebook kwa ushauri na maswali kuhusu uhusiano.



Read More
      edit

Wednesday, January 27, 2016

Published 1/27/2016 10:39:00 PM by with 0 comment

BAADA YA SALAMU NI MIZINGA, INAWAPONZA SANA KINADADA


Mada yangu ya leo inahusu moja ya tabia inayowaponza kina dada au wanawake ya kupiga mizinga kwa wapenzi wao na hata wasio wapenzi wao.

Mmoja wa wasomaji wangu alinilalamikia kuwa yeye amekumbwa na kisanga hiki baada ya kupigwa mizinga na mwanamke ambaye hana uhusiano naye wa kimapenzi zaidi ya kukutana kweye mitandao ya kijamii na kuanza kuwasiliana.

Tumsikie
Hii mitandao ina mambo sana, nilikutana na mdada mmoja tukafahamiana na kubadilisha mawasiliano, nilijua tutakuwa tunazungumza mambo ya kawaida tu lakini tulivyozidi kuzoeana ikawa kila nikimpigia baada ya kubipu ni salamu kisha mizinga.

“Dah! Wangu nimepinda mbaya, kama vipi nitoe hata twenti (20000)”.
Kama ikitokea nikamwambia sina pesa basi ataomba nimrushie vocha na tabia hii si mara moja, imezidi sana ndiyo maana nimeamua kumuuliza mtaalam wa Maisha na Mapenzi.

Athari zake
Kwa tabia hiyo ya kupiga mizingi watu hovyo imewakuta ikiwagharimu wanawake wengi kuingia katika uhusiano usio rasmi.

Inakuaje
Unapozoea kupiga mizinga mtu ambaye huna uhusiano naye wowote ni sawa na kujirahisisha mwenyewe kwa jamaa huyo, wakati mwingine jamaa anaweza kuwa hana dhamira mbaya na wewe wala hajawahi kuchezwa na mshipa dhidi yako ila kwa mizinga yako itapelekea kujenga mazoea mengine zaidi ya hayo na unajikuta ukisaliti ndoa au uhusiano wako kirahisi.

Nililolibaini
Kuna baadhi ya wanawake wanaishi mjini kwa tabia hiyo ya mizinga ya vocha kama sio vocha basi pesa, wakati ukweli ni kwamba hawana uhusiano wa karibu sana na yule anayempiga mzinga.
Ushauri wangu
Wanawake muache tabia hii kwani haipendezi na wala wanaume hawaipendi ndiyo maana inawasukuma kujiingiza katika uhusiano kiholela na wanakuwa hawana mapenzi ya kweli zaidi ya kufidia mizinga ya pesa na vocha ulizokuwa ukimpiga na kiukweli mizinga hiyo inawaponza sana.

Nikamilishe ngwe hii kwa kuwatakia wiki njema na tukutane tena wiki ijayo.

Read More
      edit
Published 1/27/2016 07:17:00 AM by with 0 comment

KUNA WANAOISHI KWA RAHA NA VIMADA KULIKO NDANI YA NDOA


Ni siku nyingine tena tunakutana katika jungu kuu lisilokosa ukoko kwa kukuletea uchambuzi  mzuri na wenye mashiko kuhusu maisha na mapenzi.

Kwa uchunguzi mdogo nilioufanya wa kuzungumza na wanaume kadhaa walio kwenye mahusiano, (hasa wana ndoa) nimegundua baadhi ya wanaume wamejikuta wakijiingiza katika maswala ya ulevi na kuchepuka (kwa kuwa na vimada) kwasababu ya karaha wanazokutana nazo kwa wake zao.

Nilichobaini wanaume wengi wanaishi kwa raha mustarehe na vimada wao  kuliko ndani ya ndoa zao. Sihalalishi kuchepuka wala kuwa na kimada ila huo ndiyo utafiti nilioufanya.

Kiasili wanaume ndiyo watafutaji wa mahitaji muhimu ya familia, jambo linalowafanya kukutana na misukosuko mingi ya kila aina; ugomvi, ushirikina, matusi, vishawishi n.k, hujitahidi kuvumilia misukosuko hiyo ili kuhakikisha anapata mkate wa siku hiyo, ili kutunza familiana yake na kuendelea kuheshimika kwa watoto na majirani kama baba mwenye kujali.

Ishu inakuja pale mwanaume anaporudi nyumbani akitegemewa kupokewa na mke wake kwa furaha, bashasha sambamba na pole ya uchovu wa kazi, lakini hali huwa si kama wanavyotegema zaidi ya kukutana na karaha kutoka kwa wanawake wao.
Wakati mwingine mmeo hutoka kazini mapema ila kila akifikiria makelele na karaha zako nyumbani, basi anaamua kukata kona kwenye baa ili angalau kupoteza muda ili akirudi  acute umelala, hilo ni tatizo.

Kama hulikuwa hujui vimada sehemu kubwa wanacheza na fursa, wanajua kuzitumia fursa ipasavyo, mumeo anapomtongoza hujua kuna kitu ambacho mumeo atakuwa amekikosa kwako, yawezekana wewe mwanamke ni mkorofi, msumbufu, mbishi, mwenye matusi, hujishughulishi na mengineyo.

Madhaifu yako dhidi ya mmeo ndiyo mafanikio na kimada, anachofanya yeye nikutumia ule udhaifu wako uliomfanya mmeo akachepukia yawezekana umeifanya ndoa yako kuwa ya mazoea, humpetipeti tena mumeo kama zamani. Umsiponjisiponji kama enzi za uchumba, umtumbui chunusi kama mlivyokuwa manatongozana  na badala yake, umegeuka dubu ndani ya nyumba.

Kwa taarifa yako mwanaume anapenda kudekezwa kama unavyopenda wewe, ila kwa karaha zako, mmeo anashindwa kutulia ndani na kuamau kutafuta vimada, yawezekana sababu zikawa ni nyingi zaidi ya hizo nilizozihainisha ila kama ni mwanamke au binti unayetegema kuingia katika uhusiano wa ndoa, jifunze, ili usije kuwa shuhuda wa haya niliyoyaandika.
Read More
      edit