Mpenzi msomaji, leo
nitaendelea na sehemu ya pili ya mada yetu hii iliyoanza wiki iliyopita ambapo
nilipokea maoni, maswali, ushauri na mengineyo ambayo baadhi yake ni kama
yafuatayo;
SARA PIUS WA MUHEZA, TANGA
Mimi na mume wangu, Alex
Kijangwa tulifunga Ndoa ya Mimba ila kwa sababu tulipendana, tumetimiza miaka
nane na upendo bado haujachuja, asante Mungu.
MKINDI, KILOMBERO
Mimi nimefunga Ndoa Yenye
Sababu mwaka 2000. Baada ya miaka saba tukawa tunaishi kwa mazoea na sijui
sababu, imetokea tu.
IRENE CAREEN, IRINGA
Mimi napenda kufunga Ndoa
ya Upendo, upendo ambao unajali utu na siyo mali.
MUNTAQ, DAR
Kwa upande wangu namuomba
Mungu anijalie nifunge Ndoa ya Upendo.
RAPHAEL, MOROGORO
Mimi napenda Ndoa ya Upendo
ingawa nyingi ziliishia mwaka 1978, ila hata sasa bado zipo sema tu ni moja
kati ya elfu moja.
GOLD ISTERN, MORO
Yote uliyoyaandika ni
ukweli mtupu big up sana, natamani sana wale ambao hawajaingia kwenye ndoa
wangepitia ukurasa huu wasome ili waelewe na si kukurupuka tu.
BAHATI, SONGEA
Ally mpenzi wangu, Ndoa ya
Upendo ndiyo inayotufaa ili tudumu miaka yote kwani nakupenda sana.
JINA KAPUNI
Asante kwa kutuelimisha,
mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 22, napenda Ndoa ya Utajiri kwani mapenzi
ya kweli hakuna kwa wanaume vijana, wengi ni pasua kichwa.
PETER WEMA WA MBEZI, DAR
Sijaolewa lakini nipo
kwenye uhusiano, nampenda mpenzi wangu napenda Ndoa ya Upendo.
JINA KAPUNI
Mungu azidi kukupa nguvu
mwandishi, napenda nifunge Ndoa ya Upendo, ndoa hizo bado zipo kama utafuata
taratibu na sheria za Mungu.
ZAWADI ZUBERI, TANGA
Napenda kufunga Ndoa ya
Upendo, siangalii pesa bali penzi la dhati.
ATHANAS, DOM
Ndoa za siku hizi ni ngumu
sana, kwani unatongoza asubuhi, jioni mnakutana faragha lakini zamani
ukitongoza leo unapewa bangili, kila ukikutana naye anakupa kitu siyo ngono
hata miaka mitatu. Lazima ndoa itangazwe ndiyo mkutane faragha.
HAPPY ANSBERT
Napenda sana ya kwangu iwe
Ndoa ya Upendo, ndiyo ndoa yenye furaha na amani mpaka mnafanana.
JINA KAPUNI
Uliyoandika nayakubali,
Ndoa za Upendo kwa sasa ni chache sana. Namuomba Mungu anijalie nipate mwanaume
atakayenipenda na tufunge ndoa hiyo.
ZENA, MWANZA
Napenda nifunge Ndoa ya
Upendo, kwani ina amani na utulivu, kama ni mali anayeleta ni Mwenyezi Mungu.
SABRINA, DAR
Kwangu mimi Ndoa ya Upendo
ni sawa kwani bila upendo hakuna ndoa itakayodumu.
MSOMAJI, DAR
Natarajia kufunga Ndoa ya
Mali yaani utajiri ili nisipate shida katika maisha yangu.
JINA KAPUNI
Ndoa nzuri, takatifu na
itakayodumu ni ya watu waliookoka, waliotii maandiko matakatifu, waliojitunza
mpaka Mungu alipowaunganisha. Ndoa yao itakuwa imejengwa juu ya mwamba imara
ambao ni Yesu Kristo.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nzuri nyingine.
Chanzo:GPL
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.