ASANTE Mwenyezi Mungu kwa kuiona siku ya leo, tunakutana tena katika kilinge chetu hiki kama ilivyo ada, bado tunaendelea kujifunza namna mbalimbali ya kufanya tunapokuwa faragha na wenza wetu. Kwa kifupi mada hii ya faragha imewavutia wengi sana ambao wameomba niendelee kuifafanua zaidi.
Nianze kwa kusema kila kitu kinahitaji hamasa au hisia ili kiweze kufanyika katika hali nzuri, ndivyo hivyo hata mapenzi nayo yanahitaji hamasa ili kuweza kuamsha hisia za mwenza wako na hatimaye kukutana faragha. Mnapokuwa faragha kuna kipindi inabidi mpongezane kwa kazi nzuri mliyoifanya ya kuhakikisha kila mtu anafurahia faragha yenu.
Leo nitazungumza kuhusu umuhimu wa vitu mbalimbali vinavyoweza kuifanya faragha yenu kuonekana ni nzuri na bora zaidi. Kuna vitu vingi ambavyo vinapaswa kufanyika ili kukamilisha faragha yenu kuwa yenye tija, baadhi yake ni kama ifuatavyo;
SAUTI YA KUBEMBELEZA
Ikumbukwe kwamba sauti ya mtu akiwa anazungumza wakati mihemko au mizuka haijampanda huwa ni sauti ya kawaida na inapotokea mihemko imepanda basi hubadilika, hiyo inayobadilika ndiyo ninayoizungumzia.
Kuna sauti f’lani za mahaba ambazo husikika watu wanapokuwa wamezama zaidi kwenye dimbwi zito la mahaba. Mfano; baadhi ya wanawake wamejaliwa kuwa na sauti f’lani za furaha au raha na zenye kuhamasisha wanapokuwa faragha na wenza wao, kiukweli sauti hizo zinastahili kuwepo ili kumhamasisha mwenza wako.
Sauti hizo za mahaba siyo tu kwa wanawake, hata kwa wanaume pia.
Kusikika kwa sauti hizo za mahaba hata kama mwenza wako atakuwa amechoka pindi anapozisikia au kuzifikiria sauti zile akilini mwake basi anapata nguvu mpya ya kuingia tena ulingoni.
Japokuwa kila mwanadamu ameumbwa na aina yake ya hamasa anapokuwa faragha, kwa hiyo kama hatakuwa na sauti za mahaba, basi anaweza kuwa na kitu kingine zaidi.
Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook na WhatsApp kujua mengi kuhusu mapenzi.
Mada hii itaendelea wiki ijayo.
MAMBO YANAYOFURAHISHA FARAGA-2
Watanzania tunu yetu kubwa tuliyojaliwa na Mungu ni amani, amani ndiyo imenifanya leo uweze kusoma mada hii ya mambo yanayofaa faraghaWiki iliyopita tulizungumzia kipengele kimoja cha sauti za kubembeleza leo nitaendelea na mambo mengine mazuri mnapokuwa faragha;
BUSU
Kama ulikuwa hujui busu ni zuri mnapokuwa faragha kwani linahamasisha sana kinyang’anyiro chenu, wakati mwingine ukipiga busu lililozuri linaweza kuwa ni kumbukumbu kwa mwenza wako kwa muda mrefu.
DEKO
Kudeka hasa unapokuwa faragha ni poa sana kwani inaonesha ni namna gani unajisikia furaha, amani, upendo kuwa na mtu ambaye ukimdekea anakufariji na kukubembeleza, ni nzuri hii kwa uhusiano, haijalishi cheo chako, umri au uwezo ulionao.
MINONG’ONO
Sauti za mahaba huwa ni zile za kunong’onezana zenye kujaa matamshi ya kubembelezana, minong’ono hiyo huhamasisha sana mnapokuwa faragha hasa baada ya kumaliza ngwe ya kwanza na kuitafuta ya pili.
Pongezi
Wengi hujisahau sana kutoa pongezi kwa wapenzi wao mara baada ya kumaliza tendo husika na matokeo yake wanakuwa kama vile wana ugomvi, mkimaliza kazi mwambie mpenzi wako, baby pole kwa kazi nzito uliyofanya.
FURAHIA
Pongezi pekee hazitoshi kama unahisi umefurahia huduma yake , mwambie kabisa ili na yeye ajue amefanya kazi nzuri aliyopaswa kufanya na hata kama hajafanya vizuri mwambie ukweli ‘ ila mai kwa leo mimi sijainjoi wangu, haikuwa kama siku ile…’’
VALISHANENI
Kama mliweza kushirikiana mwanzoni mwa zoezi kwa kusaidiana kutoa sehemu ya nguo zenu, vivyo hivyo mnapaswa kushirikiana pia katika kuvalishana mara baada ya kumaliza zoezi lenu.
Kimsingi mapenzi ni uwezo binafsi lakini pia ni suala la utundu na ujanja wa mtu katika kuhakikisha anaweza kumfikisha mwenza wake mahali anapohitaji kufika kwa maana ya kufikia kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Mpenzi msomaji usikose mada nyingine tamu wiki ijayo, pia usikose kufuatilia ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook na WhatsApp kujua mengi kuhusu mapenzi.
Na Gabriel Ng’osha-GPL
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.