Mpenzi msomaji, tukubaliane kuwa maisha ni kuchagua. Je, ulishawahi kujiuliza unapenda kuoa au kuolewa ndoa ya aina gani? Bila shaka jibu unalo.
Zifuatazo ni baadhi ya ndoa katika jamii yetu, bila shaka kati ya wasomaji wangu wapo waliozipitia na wengine wakitamani wafunge ndoa za namna hii;
1: NDOA YA MKEKA
Hii ni ndoa ambayo hutokana na kijana kufumaniwa na binti wa watu. Mara nyingi ndoa hii huvunjika mwaka mmoja tu baada ya wanandoa kugundua hawakuwa wakipendana kwa dhati!
2: NDOA YA MIHEMKO
Aina hii ya ndoa hufungwa na vijana wenye umri mdogo, mtoto wa kiume kati ya miaka 18 hadi 20 na 16 hadi 18 kwa mtoto wa kike. Ndoa hii inawezekana kuvunjika baada ya miaka mitatu au minne.
4: NDOA YA MAONESHO
Wenye ndoa hii hupenda kujionesha ufahari mitaani na barabarani. Ila ukiingia ndani yake, hazina utii. Mara nyingi wahusika hukwaruzana na kupigana mara kwa mara. Cha kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa zinazoongoza kwa michepuko!
5: NDOA YA UHAMISHO
Ndoa hii hufungwa na watu wa vijijini na mjini ambapo wa kijijini hulazimika kuhamia mjini kwa maana ya kumfuata mwenza wake. Hii ni moja ya ndoa zenye ukakasi na hue nda ikavunjika mara tu wanapoanza kuishi wote mjini.
6: NDOA YA MIMBA
Ndoa hii hufungwa kwa sababu wanaooana hawataki kuonekana kwao kuwa wamezaa nje ya ndoa. Wakati mwingine muolewaji alikuwa hampendi mwenza wake kwa dhati au familia yake haimpendi. Muoaji hutumia mimba kama mtego wa kuingia katika ndoa. Hii huvunjika mara tu mtoto anapozaliwa na kufikisha umri wa mwaka mmoja.
7: NDOA YA MALI (UTAJIRI)
Muolewaji huwa ni wa umri wa miaka kati ya 18 hadi 28 na muoaji anaweza kuwa na umri hata kati ya 65 hadi 70. Ndoa ya aina hii hudumu kwa sababu mwenye kauli ni mwenye mali. Lakini pia uwezekano wa muolewaji kuchepuka ni mkubwa.
8: NDOA YENYE SABABU
Ndoa hii hufungwa ilimradi muoaji au muolewaji aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au kaolewa. Huwa hazina utii wala upendo wa dhati. Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka minne huwa hazivunjiki, wahusika huishi kwa mazoea.
9: NDOA YA UPENDO
Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya Vita vya Kagera (kati ya Tanzania na Uganda). Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote.
10: NDOA YA KUCHUMA
Ndoa hii hufungwa ilimradi muoaji au muolewaji apate kitu au vitu fulani kutoka kwa upande mmoja. Mpenzi msomaji tuma maoni yako kuhusu ndoa unayotarajia kufunga au uliyofunga wiki ijayo yatakuwa hapa.
Gabriel Ng’osha-GPL
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.