Ni siku nyingine tena tunakutana katika jungu kuu lisilokosa ukoko kwa
kukuletea uchambuzi mzuri na wenye mashiko
kuhusu maisha na mapenzi.
Kwa uchunguzi mdogo nilioufanya wa kuzungumza na wanaume kadhaa walio
kwenye mahusiano, (hasa wana ndoa) nimegundua baadhi ya wanaume wamejikuta
wakijiingiza katika maswala ya ulevi na kuchepuka (kwa kuwa na vimada)
kwasababu ya karaha wanazokutana nazo kwa wake zao.
Nilichobaini wanaume wengi wanaishi kwa raha mustarehe na vimada wao kuliko ndani ya ndoa zao. Sihalalishi
kuchepuka wala kuwa na kimada ila huo ndiyo utafiti nilioufanya.
Kiasili wanaume ndiyo watafutaji wa mahitaji muhimu ya familia, jambo
linalowafanya kukutana na misukosuko mingi ya kila aina; ugomvi, ushirikina,
matusi, vishawishi n.k, hujitahidi kuvumilia misukosuko hiyo ili kuhakikisha
anapata mkate wa siku hiyo, ili kutunza familiana yake na kuendelea kuheshimika
kwa watoto na majirani kama baba mwenye kujali.
Ishu inakuja pale mwanaume anaporudi nyumbani akitegemewa kupokewa na mke
wake kwa furaha, bashasha sambamba na pole ya uchovu wa kazi, lakini hali huwa
si kama wanavyotegema zaidi ya kukutana na karaha kutoka kwa wanawake wao.
Wakati mwingine mmeo hutoka kazini mapema ila kila akifikiria makelele
na karaha zako nyumbani, basi anaamua kukata kona kwenye baa ili angalau
kupoteza muda ili akirudi acute umelala,
hilo ni tatizo.
Kama hulikuwa hujui vimada sehemu kubwa wanacheza na fursa, wanajua
kuzitumia fursa ipasavyo, mumeo anapomtongoza hujua kuna kitu ambacho mumeo
atakuwa amekikosa kwako, yawezekana wewe mwanamke ni mkorofi, msumbufu, mbishi,
mwenye matusi, hujishughulishi na mengineyo.
Madhaifu yako dhidi ya mmeo ndiyo mafanikio na kimada, anachofanya yeye
nikutumia ule udhaifu wako uliomfanya mmeo akachepukia yawezekana umeifanya
ndoa yako kuwa ya mazoea, humpetipeti tena mumeo kama zamani. Umsiponjisiponji
kama enzi za uchumba, umtumbui chunusi kama mlivyokuwa manatongozana na badala yake, umegeuka dubu ndani ya
nyumba.
Kwa taarifa yako mwanaume anapenda kudekezwa kama unavyopenda wewe, ila
kwa karaha zako, mmeo anashindwa kutulia ndani na kuamau kutafuta vimada,
yawezekana sababu zikawa ni nyingi zaidi ya hizo nilizozihainisha ila kama ni
mwanamke au binti unayetegema kuingia katika uhusiano wa ndoa, jifunze, ili
usije kuwa shuhuda wa haya niliyoyaandika.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.