Basi baada ya Mery kupewa kipigo hevi na mama yake
mwisho alifunguka kuwa pamoja na kusumbuliwa na Kangasu ila hajawahi kumpa
tunda spesho zaidi ya kumzungusha.
Hata hivyo kuna mwanafunzi mwingine ambaye amekuwa kero
sana kwake kwa kumsumbua.
“Eeh! Nani huyo tena?” mwalimu mmoja alidakia kuuliza swali.
“Huwezi amini ni mwanafunzi wenu ambaye huwa mnamuona ni
mpole, mwenye na adabu,” kabla hata ajamalizia.
“Magambo huyo.”
“Duh! Haya makubwa sasa.”
Usichoke wakati sijamalizia kukuhadithieni, mwalimu
Mtanange aliwaambia mkwa Magambo kuna kisa kilichopelekea kuanza kumsumbua Mery
huwezi kuamini kisa ni zile peni za bomba nne ambazo unakuta zina wino mweusi,
bluu, kijani na nyekundu.
Mmoja wa walimu hao akahamaki kwa kuuliza swali, peni
hiyo imefanyaje?
Nyie tulieni mbona mnanichamba wakati sijamaliza kujisaidia
mwalimu alijibu kwa utani, inasemekana Magambo alimuazima Mery kalamu yake ya
bomba nne ili afanyie mtihani kisha airudishe kwa mwenyewe ila inavyoonekana ni
kama Mery aliipoteza ile kalamu ya Magambo, kwani kila alipokuwa kaiombwa ile
kalamu anamzungusha kila siku, mwisho wa siku Magambo akamwambi Mery kama ni
hivyo wamalizane kwa kumpa ‘mnyengo’
‘Mnyengo’ ndiyo nini? aliuliza mwalimu mmoja wa kike
aliyekuwa shuleni pale kwa majaribio baada ya kutoka chuoni.
‘Mnyengo’ akimaanisha mapenzi, du hawa watoto wana mambo
sana wanajifunzia wapi, hayo mambo?
Itakuwa kwenye masinema yao huko mitaani, alidakia
mwalimu mwingine.
Kwahiyo Magambo akaendelea kumsumbua Mery kwa muda mefu akitaka
‘mnyengo’ sema akawa mgumu kuutoa.
Alafu cha
kushangaza sasa kalamu hiyo insemekana Magambo alimuazima Mery toka mwaka jana wakati
ule tukiwa bado tuko kwenye shule ile ya udongo tuliyohama.
Sasa kajamaa na kenyewe kamekomaa kumdai tu na yeye hataki kulipa.
“Haaahaa haaa haaa ! Walimu wajikuta wakigongana
mikononi , haswa baada ya kusikia tunda likiitwa jina ambalo hata wao na ualimu
wao ni jina geni.
Kiukweli nilivyoasimuliwa na mama yule nilisikitika sana
kwani niliona kama walimu wote tumevuliwa nguo, inakuaje vijana hawa wadogo
wanaanza mambo ya wakubwa haraka hivi wakati wako darasa la sita?
Nini
kilifuatia usikose wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.