Mada yangu ya leo inahusu moja ya tabia inayowaponza
kina dada au wanawake ya kupiga mizinga kwa wapenzi wao na hata wasio wapenzi
wao.
Mmoja wa wasomaji wangu alinilalamikia kuwa yeye amekumbwa
na kisanga hiki baada ya kupigwa mizinga na mwanamke ambaye hana uhusiano naye
wa kimapenzi zaidi ya kukutana kweye mitandao ya kijamii na kuanza kuwasiliana.
Tumsikie
Hii mitandao ina mambo sana, nilikutana na mdada mmoja
tukafahamiana na kubadilisha mawasiliano, nilijua tutakuwa tunazungumza mambo
ya kawaida tu lakini tulivyozidi kuzoeana ikawa kila nikimpigia baada ya kubipu
ni salamu kisha mizinga.
“Dah! Wangu nimepinda mbaya, kama vipi nitoe hata twenti
(20000)”.
Kama ikitokea nikamwambia sina pesa basi ataomba
nimrushie vocha na tabia hii si mara moja, imezidi sana ndiyo maana nimeamua
kumuuliza mtaalam wa Maisha na Mapenzi.
Athari
zake
Kwa tabia hiyo ya kupiga mizingi watu hovyo imewakuta
ikiwagharimu wanawake wengi kuingia katika uhusiano usio rasmi.
Inakuaje
Unapozoea kupiga mizinga mtu ambaye huna uhusiano naye
wowote ni sawa na kujirahisisha mwenyewe kwa jamaa huyo, wakati mwingine jamaa
anaweza kuwa hana dhamira mbaya na wewe wala hajawahi kuchezwa na mshipa dhidi
yako ila kwa mizinga yako itapelekea kujenga mazoea mengine zaidi ya hayo na unajikuta
ukisaliti ndoa au uhusiano wako kirahisi.
Nililolibaini
Kuna baadhi ya wanawake wanaishi mjini kwa tabia hiyo ya
mizinga ya vocha kama sio vocha basi pesa, wakati ukweli ni kwamba hawana
uhusiano wa karibu sana na yule anayempiga mzinga.
Ushauri
wangu
Wanawake muache tabia hii kwani haipendezi na wala
wanaume hawaipendi ndiyo maana inawasukuma kujiingiza katika uhusiano kiholela na
wanakuwa hawana mapenzi ya kweli zaidi ya kufidia mizinga ya pesa na vocha
ulizokuwa ukimpiga na kiukweli mizinga hiyo inawaponza sana.
Nikamilishe ngwe hii kwa kuwatakia wiki njema na
tukutane tena wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.