Monday, February 29, 2016

Published 2/29/2016 08:24:00 PM by with 0 comment

TAMBUA WANAKUPENDA KWA SABABU UKO KWANGU!


ASANTE Mungu kwa Jumatatu nyingine murua, umenipa uhai, afya, nguvu na mengineyo yote ni kwa uweza wako. Mpenzi msomaji baada ya wiki mbili za machungu yaliyotokana na mada ya wale waliopoteza wapenzi au wapendwa wao, leo tunazungumzia namna ambavyo wapenzi wengine wamekuwa wakithaminiwa na wapenzi wao lakini wao hawathaminiki kwa sababu tu wanaume au wanawake wengi mtaani huwatamani na kusahau kuwa anayempenda ni mmoja tu na ndiye pengine aliyemchumbia au kufunga naye ndoa.

Wapenzi wengi wamejikuta wakihadaika sana na wapenzi walio nje ya uhusiano wao na kuwasahau waliowachagua na kuishi nao kama wenza wao. Wengi wamejikuta wakiangukia pua kwa kuchepuka na wapenzi ambao kwa uhakika wanakuwa si sahihi kwani waliosahihi ni wale tu waliowathamini na kuwaweka ndani.

Ukitaka kuamini ninachokisema, hebu jaribu kujitoa kwa aliyekuthamini na kukuweka ndani kisha uone kama yule uliyekuwa unachepuka naye ataweza kukuhudumia na kukupendezesha kama ambavyo ulikuwa na mchumba, mume au mke?
Mthamini na mpende yeye aliyekufikisha hapo, haijalishi ni magumu mangapi ambayo mmekutana nayo, usipende vitu vya bure na starehe za hapa na pale kutoka kwa wachepukaji. Aliyekuweka ndani ana nia nzuri na wewe na ndiyo maana amekuchagua uwe mwandani wake.
Pata japo nafasi ya kumwambia mwandani wako: “Tambua kuwa huyo bwana au mwanamke anakupenda tu kwa sababu uko kwangu, akiuona muonekano wako na jinsi hiyo shepu yako ilivyo, basi anakutamani na si kukupenda kama nikupendavyo mimi, kukuthamini kama ninavyokuthamini, nilikupenda na nilitambua thamani yako ndiyo maana nimekuweka ndani.

“Wazuri ni wengi sana dunia hii ila ninaamini siwezi kuwamaliza na ndiyo maana nilikuchagua wewe wa kipekee ambaye nitakupenda, nitakujali, nitakulinda na kukuthamini hadi kifo kitutenganishe.
“Yawezekana ulinikosea kwa kunisaliti, sitamani niyajue hayo bali ninakuomba ujirekebishe mpenzi wangu maisha yaendelee.

“Ninaamini kabisa wanaokutamani na kukutaka wapo wengi sana lakini sina uhakika kama usingekuwa kwangu wangekutamani kama ambavyo wanafanya kwa sasa, hawajui ni wapi tulikotoka, wanakutamani kwa sababu wanakuona ukiwa umependeza kwa nguo nadhifu nilizokuandalia, haukuwa hivi kipindi kile.
“Haukuwa umeng’ara kama ulivyo sasa, utanashati wako unawachanganya wengi, tafadhali, tulia na mimi kwani wewe ndiye faraja ya kweli ya maisha yangu, mimi ndiyo nuru ang’avu ndani ya mboni ya jicho lako lililokuwa limejaa giza.

“Nakujali na kukupenda kwa sababu tu umenipa nafasi ya kujua siri na udhaifu wako wa ndani, najua nini nikikifanya unafurahia, nafahamu nini nikikosea unachukia, tafadhali, usiwape nafasi wengine kwani wewe ndiye tunda langu lenye raha tele maishani mwangu. Ninaamini hao wengine wanakutamani tu kwa sababu ya matunzo ninayokupa. Najua wanakutamani kwa sababu ya muonekano wako ambao sehemu kubwa umechangiwa na matunzo na malezi yangu kwako.”


Usikose wiki ijayo kwenye mada nyingine tamu, pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamiii wa Facebook, Insta:@mimi_na_uhusiano au tuna namba tukuunge kwenye group letu la WhatsApp.
Read More
      edit
Published 2/29/2016 06:28:00 AM by with 0 comment

HABARI ZA MAGAZETI YA FEB, 29






Read More
      edit
Published 2/29/2016 06:11:00 AM by with 0 comment

WALIMU KUPANDA DALADALA BURE DAR



MANENO YA DC PAUL  MAKONDA; Kwa ufupi ni kwamba, wazo hili limejengwa juu ya msingi wa sababu kubwa tatu. Moja, kwa kuzingatia changamoto za nauli za mara kwa mara wanazolazimika kuzilipa walimu ili kuyafikia kwa wakati maeneo yao ya kufanyia kazi na pili, ni kuhakikisha mimi na serikali yangu ya wilaya ya Kinondoni tunakuwa sehemu ya juhudi za Mheshimiwa Raisi za kuboresha maslahi na mazingira ya walimu ya kufanyia kazi ili matarajio ya ndoto yake anayoipigania usiku na mchana ya kutaka kuiona sekta ya elimu nchini ikikua kwa kasi yanatimia.



Na tatu, ni kuwafanya walimu wa wilaya ya Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla kama watumishi wenzangu wa serikali nao wanafaidi sehemu ya matunda ya serikali yao ambayo kwa dhati imedhamiria kubadilisha maisha yao ili na wao waweze kubadilisha maisha ya vijana wetu kupitia taaluma.
Kwasababu hizo nilizozianisha hapo juu ninaomba kuwatangazia walimu wangu wa shule zote za serikali kuanzia za msingi mpaka sekondari ya kwamba, sasa watasafiri bure wanapokwenda kutufundishia wadogo zetu na watoto wao. 


Hii ni baada ya kufanya vikao na mazungumzo ya kina na wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma kupitia vyama vyao vya Darcoboa na Uwadar na hatimaye mazungumzo hayo kuitimishwa na mkutano wa vyama vyote hivyo viwili vya wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao kwa sauti moja wamekubali kuniunga mkono kwenye utekelezaji wa wazo langu hili.
Kipekee na kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wamiliki hawa wa vyombo vya usafiri wa umma pamoja na viongozi wa vyama vya Darcoboa na Uwadar kwani walikuwa na kila sababu ya kukataa hasa ukizingatia kuwa wao ni wafanyabiashara na tena wanazo changamoto nyingi katika sekta yao ya usafirishaji, wengine wakiwa hata wamekopa kwenye mabenki ili wapate uwezo wa kufanya biashara, lakini kwenye jambo hili wote kwa umoja wao wameseme ndio na wako tayari kuanza haraka iwezekanavyo.

Utaratibu kwa walimu juu ya utumiaji wa fursa ambayo tumeipata utakuwa kama ifuatavyo:- Moja, nimemuelekeza ofisa elimu wa sekondari na shule za msingi, kutoa maelekezo kwa wakuu wa shule zote za serikali zilizopo wilayani kwangu na wilaya nyinginezo za jiji la Dar es Salaam, kutengeneza vitambulisho vya shule zao vitakavyokuwa na picha ya mwalimu, jina lake kamili, jina la shule anayofundisha, namba ya simu ya mkuu wa shule husika pamoja na saini yangu mimi mwenyewe Paul Makonda ili kuepuka udanganyifu.
Nimewataka zoezi hili walifanye na kulikamilisha ndani ya wiki moja ambapo baada tu ya kukamilika itakuwa ni furaha yangu kuwatangazia walimu wote wa shule za serikali jijini Dar es Salaam kuwa, watakuwa wakipanda daladala bure ila tu kwa siku za jumatatu mpaka Ijumaa na kwa muda wa saa kumi na moja asubuhi mpaka saa mbili asubuhi na kati ya saa tisa mpaka saa kumi na mbili jioni. Ingawa, kila mwalimu atalazimika kuonyesha kitambulisho chake alichotengenezewa kwenye shule yake pamoja na kile cha ajira ya serikali.


Read More
      edit

Sunday, February 28, 2016

Published 2/28/2016 07:59:00 PM by with 0 comment

PANYA ALIVYONISUMBUA KWA SIKU 20



ilipoishia
Nilirudi haraka kitandani baada ya kusikia simu yangu ikinguruma, mawazo yangu yote nikijua lazima Lydia atakuwa amenijibu kitu, mapigo ya moyo yakaanza kunienda kwa kasi maana jinsi ninavyompenda huyu mtoto Mungu mwenyewe ndiye anayejua.


03.
Tofauti kabisa na nilivyofikiria ujumbe ule haukuwa wa Lydia bali ulikuwa wa Tigo ukinikumbusha kulipa mkopo wa nipige tafu. Nilipochungulia simu ya Lydia niliona bado ipo online halafu safari hii amebadilisha na picha yake ya profile amemweka huyo bwana ake Boniface huku status yake ikosomeka: wenye wivu wajinyonge;  sijui alikuwa akinilenga mimi?

Nilikasirika kwa kweli, safari hii nikazima taa na kujitupa kitandani na kujikuta nikizama kwenye lindi la mawazo kuhusu maisha yangu kwa ujumla, jinsi nilivyotoka kijijini na kuanza maisha ya kuhangaika mjini na hatimaye kupata kazi ya kufagia kwenye kampuni maarufu ya Jambo Freight.

Mwanzoni nilikuwa nikiishi kwa shida sana kuanzia kula hadi kulala lakini baada ya kuwekeza mishahara yangu ya miezi mitatu sasa na mimi nimeweza kupanga na kuondokana na lawama za marafiki.
Lakini cha ajabu wakati mimi hayo nikiyaona ni mafanikio, mpenzi wangu Lydia hayaoni kabisa na amedata kweli na muuza chipsi wa Africasana, kwa kweli inauma lakini bado sijakata tamaa.

Nilishusha pumzi na kutazama vizuri chumba changu nilitazama kuanzia paa lake ambalo lilionesha kuwa nyumba ile ni ya zamani maana mabati yake yaliyochakaa yalishikiliwa na miti ya mtalawanda, nilipotazama kuta za chumba kile nilishangaa kuona kikifanana kabisa na kile chumba nilichokiota ndotoni.
Nilishtuka na kuanza kuutafuta ule ufa na lile shimo, nililoliota, kweli niliuona na lile shimo dogo aliloingia yule panya mwanzoni, nilistaajabu sana kwa hilo, nikarudi zangu kulala nikiwa na hofu huenda nimeingia kwenye chumba cha mauzauza kama wanavyosimuliaga wenzangu.
Je, nini kitaendelea usikose kufuatilia..
Read More
      edit
Published 2/28/2016 08:25:00 AM by with 0 comment

JUMAPILI NJEMA

 

Asante MUNGU kwa kuwa umetuzawadia kuweza kuiona siku hii ya leo, hakika wewe ni mwema kwetu. Na Mlapa Ng'osha.





Read More
      edit
Published 2/28/2016 08:15:00 AM by with 0 comment

HABARI MAGAZETINI FEB, 28/2016



























Read More
      edit
Published 2/28/2016 08:04:00 AM by with 0 comment

YAWEZEKANA UMEMPOTEZA MWANAO, SOMA HAPA


2 Samweli 12:22-23
Daudi akawajibu, “Ni kweli mtoto alipokuwa hai, nilifunga na kulia, nani anajua? Huenda Mwenyezi-Mungu akanirehemu ili mtoto aishi’. Lakini sasa amekufa, ya nini nifunge? Je, mimi naweza kumrudisha duniani? Siku moja, nitakwenda huko alikokwenda, lakini yeye hawezi kurudi kwangu.’’
Read More
      edit

Saturday, February 27, 2016

Published 2/27/2016 09:40:00 PM by with 0 comment

BAYO NA IMBORI-1

     
HALI ya hewa siku hiyo ilikuwa ya baridi sana kama ilivyozoeleka katika mji wa Manyara kiasi cha kufanya maeneo mengi kutulia tuli huku purukushani za kila siku zikiendelea kama kawaida.
Msichana Imbori alionekana mwenye majonzi mengi mbele ya baba yake mzazi Chifu Rohay Bariwe kwani siku hiyo ya Aprili 5, 1994  alitakiwa kufukuzwa mbele za watu  waliokuwepo nyumbani kwao hapo kwa kiongozi wao ili kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Miongoni mwa watu wote waliokuwepo  ni Isara, mke wa pili wa chifu Rohay Bariwe na mama mzazi wa Imbori na Marmo.
Kama ilivyokuwa kwa Imbori, Isara pia alikuwa mwingi wa huzuni, alilia sana akiwa  amemfumbata miguuni mwake mwanaye wa miaka sita aitwaye Marmo aliyekuwa akimshuhudia Imbori akifungashiwa mizigo michache ili kufukuzwa katika jamii hiyo ya Kabila la Wairaqw baada ya kukiuka miiko ya utamaduni.
Moyo ulikuwa unamuuma mno mwanamke Isara kwa sababu baada ya hapo hakukuwa na matumaini ya kumuona tena mwanaye mpendwa Imbori! Kama si kufa kwa kuliwa na wanyama wakali basi angeuawa na makabila ya watu walioishi msituni kwa kula nyama zikiwemo za binadamu.

“Kwa nini wasimsamehe tu!” msichana mmoja alisikika akimwambia jirani yake kwa masikitiko.
“Watajiletea matatizo kwenye familia yao.”
“Masikini Imbori!”
Watu wengi walionekana kugubikwa na majonzi kuliko kawaida, lakini ukweli ni kwamba hakukuwa na namna yoyote ya kulizuia jambo hilo! Imbori alifungashiwa mahindi ya kuchoma ndani ya furushi dogo, nyama-choma pamoja na karanga zilizobabuliwa kwenye moto. 

Akatakiwa kuondoka nje kabisa ya kijiji cha Luqandamuru kilichopo ndani ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
“Mama na Marmo kwa herini, ninasikitika sitawaona tena...”
“Dada usiniachee  nakupenda sana...Dadaaa...” Marmo alichomoka mikononi mwa mama yake huku akipiga kelele za uchungu, akakimbia mpaka pale alipokuwa Imbori na kumkumbatia kwa nguvu hadi wakadondoka chini.
Kila mmoja alikuwa anafuta machozi! Ni ukweli kwamba walimpenda sana msichana huyo hasa kwa ustadi wake mkubwa wa kuimba nyimbo za majonzi kipindi cha kuwaaga mashujaa waliokuwa wanakwenda vitani kupambana na makabila yenye uadui na kabila lao.  Lakini hakukuwa na namna, kila aliyekwenda tofauti na utamaduni wao alitakiwa kutendewa hivyo.

“Kamtoeni huyo mtoto!” chifu Rohay Bariwe aliwaamuru walinzi wake kwa ujasiri huku akifuta machozi pia.
“Niacheni! Niacheni! Niacheee...” Marmo alijitahidi kufurukuta lakini alizidiwa nguvu, akarudishwa kule alikokuwa amekaa mama yake mzazi Isara.
   ***
Baada ya Marmo kuondolewa, Imbori aliinuka na furushi lake mkononi akaanza kupiga hatua za taratibu huku akisindikizwa na macho ya wanakijiji wenzake waliompenda mpaka pale alipotokomea kabisa kwenye upeo wa macho yao.
Nyuma yake aliacha minong’ono na vilio vingi! Wengi wa wasichana waliohudhuria katika tukio hilo walilaani juu ya mila na desturi za kabila lao wakisema, ziliwanyima haki ya msingi ya kuomba msamaha pale ambapo walikuwa wakidondokea kwenye makosa ambayo binadamu yeyote angeweza kufanya.
“Hizi mila haziwatendei haki wasichana wetu,” Qorro rafiki yake kipenzi na Imbori aliwaza huku machozi yakimmwagika.
***
Mwishowe saa nane zilikatika Imbori akivuka mabonde na milima, hatimaye majira ya saa 12 za jioni alikuwa ndani ya msitu wa Dakwii ulioaminika kutunza wanyama wakali wa porini lakini pia msitu huo ulikuwa unapakana na Kijiji cha Magara kwa upande wa kaskazini, kulikoishi jamii ya kabila la Wadatoga.
“Nakufa Imbori!” aliwaza msichana huyo huku akizidi kutembea, mashavuni kwake machozi yalikuwa yanabubujika kwa wingi.
Wakati huo giza lilikuwa limeanza kutanda katika anga la msitu huo, kwa mbali Imbori  alianza kuzisikia sauti za ndege na wanyama asiowaelewa.
Ghafla mapigo ya moyo wake yalianza kwenda mbio lakini hakuwa na jambo la kufanya zaidi ya kupiga moyo konde, akazidi kusonga mbele kwa ujasiri mkubwa, giza lilipozidi alitafuta mti uliomfaa akapanda ili ajisitiri kwa lengo la kuendelea na safari yake siku iliyofuata.
Akiwa juu ya mti huo, Imbori alijikuta akizama kwenye dimbwi zito la mawazo. Alikuwa anaiwaza familia yake, safari mpya ya maisha aliyokuwa ameianza.  Alimkumbuka pia mpenzi wake Bayo ambaye kwa wakati huo hakuwa anafahamu kuwa alikuwa hai au la!
                                     USIKOSE SEHEMU INAYOFUATIA
Read More
      edit

Thursday, February 25, 2016

Published 2/25/2016 06:39:00 AM by with 0 comment

HABARI ZA MAGAZETI FEB, 25/2016






















Read More
      edit