Sunday, February 14, 2016

Published 2/14/2016 01:33:00 PM by with 0 comment

PANYA ALIVYONISUMBUA KWA SIKU 20

SIKU YA KWANZA
01.
Nikiwa nimechoka kwa kuhamishia mizigo yangu kwenye chumba kipya nilichopanga maeneo ya Kijitonyama Alimaua, pale karibu kabisa na kituo cha Polisi, nilijikuta nikipitiwa na usingizi mzito sana.
Ndani yake nikaota ndoto ya ajabu ambayo mpaka nilivyoamka siku ya pili yake nilipoikumbuka tu nilihisi kusisimka.
Ndoto yenyewe ilikuwa hivi:
Nilikuwa peke yangu chumbani, ghafla niliona tundu kubwa likifunguka kutokea kwenye ufa mdogo uliopo pembeni ya ukuta wa chumba kile.
Mara lile tundu lilikuwa kubwa kiasi cha kujaa ukuta mzima halafu ndani yake kukatokea kiumbe cha ajabu chenye sura ya mtu lakini meno yake na masikio yalifanana kabisa na panya buku.
Kiumbe hiki chenye macho makali kilikuja mpaka karibu na kitanda changu na kunusa huku na huko mara kikapanda kitandani kwangu na kuanza kunitafuna miguu yangu. Nililia kwa maumivu makali lakini cha ajabu sikuweza kujinasua wala kutikisika..

Je nini kilimtokea kwenye ndoto hiyo..
Itaendelea..
      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.