Ilipoishia..
Kiumbe hiki
chenye macho makali kilikuja mpaka karibu na kitanda changu na kunusa huku na
huko mara kikapanda kitandani kwangu na kuanza kunitafuna miguu yangu. Nililia
kwa maumivu makali lakini cha ajabu sikuweza kujinasua wala kutikisika..
Endelea..
02.
Baadaye
nilishtuka lakini ilikuwa ni usiku mnene. Cha kushangaza kila nilipotaka kulala
tena nilishindwa kabisa na wala siku na lepe la usingizi.
Niliamua
kuwasha simu yangu na kumtumia meseji kwa whatsapp mpenzi wangu Lydia kwa
sababu hadi muda huo wa saa 9 usiku mtandao wake ulionesha alikuwa online.
Lakini kila
nilipomtumia meseji zangu nilishangaa baada ya kuona akikaa kimya. Niliumia
sana kwa sababu nilijua tu lazima atakuwa akichati na yule mpenzi wake wa
zamani, Boniface maana nilishamfuma mara kibao lakini alikuwa akijitetea.
Kutokana na
kukosa cha kufanya, niliamua kukitazama vizuri kile chumba, niliamka na kwenda
kuwasha taa lakini ghafla nilihisi kitu kikikimbia kwa kasi na kupotelea nyuma
ya sofa langu nililoliegesha kihasarahasara upande huo.
Nilisogea
hadi kwenye lile kochi lakini nishangaa baada ya kuona mkia wa panya
ukimalizikia kutoka kwenye shimo dogo lililokuwepo kwenye kona ya ukuta huo.
Nilirudi
haraka kitandani baada ya kusikia simu yangu ikinguruma, mawazo yangu yote
nikijua lazima Lydia atakuwa amenijibu kitu, mapigo ya moyo yakaanza kunienda
kwa kasi maana jinsi ninavyompenda huyu mtoto Mungu mwenyewe ndiye anayejua.
Itaendelea..
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.