Tabia hii ya wanawake wengi ya kutaka au kukimbilia kuolewa si jambo baya, kama ikitokea ukapata bahati hiyo ya kuolewa lakini kama haitatokea sio ishu sana bali kumbuka kuwa kuna maisha nje ya kuolewa nayo si mengine ni maisha ya kufikia ndoto zako.
Kama haujaolewa
Ni kweli Mungu alituumba na kutuweka duniani ili tuujaze ulimwengu lakini hata hilo la upande wa pili nalo ni la kushukuru pindi linapokukuta, linauma ila kupunguza maumivu yake ni kulikuba li na kujifunza vitu vingine vingi ili uweze kuendelea na maisha mengine.
Hulka ya wanawake
kuolewa imekuwa ni sehemu ya wengi wao, utamsikia binti wa miaka 16 amemaliza darasa la saba anataka kuolewa eti kisa amefeli mtihani wa mwisho, wewe nani kakuambia ukifeli mtihani wa drasani ndiyo umefeli maisha? Umefeli kutimiza ndoto zako?
Kukosa bahati
Kuna wakati naamini wanawake wanakosa fursa au bahati ya kusaidiwa vitu f’lani na mwanaume anayekuwa naye, kwa kuhofia ataambiwa kuoa wakati huo pengine yeye hana uwezo huo.
Nje ya ndoa Lengo
langu si kukufanya wewe mwanamke usiolewe bali ni kukukumbusha kuwa kuna mambo mengine zaidi ya hilo. Kuolewa sio ndoto ni wajibu ambao Mungu ameuweka kwa wanadamu pindi watakapoafikiana ila kila mtu ana ndoto zake.
Usisahau ndoto zako
Wanawake wengi wamekuwa wakilisahau hilo la ndoto, wamesahau pindi walipokuwa wanasoma na walipoulizwa kuwa wakikuwa wanapenda kuwa akina nani? Najua wewe unayesoma mada hii ulisema unataka kuwa mtetezi wa wanawake, kuna mwingine alisema anataka kuwa mwanasheria, rais, mwalimu, mwanasayansi, rubani na kadhalika, sasa nashangaa leo ndoto zako zote zimeyeyuka kinyemela hivyo?
Acha mawazo mgando
Funguka kama ikitokea hujabahatika kutokuolewa usijilaumu na kujiona kama una mkosi vile, lahasha! bado unaweza kutimiza ndoto zako, ndoto zinapiganiwa, ndoa ni maridhiano na makubaliano.
Mada hii haihalalishi nwanaume kuendekeza tabia ya kutaka kukutana faragha mwenza wake bila kufikia malengo ya kuoana kwani ni tendo lenye baraka na ni muhimu sana kama utafanikiwa ila kutimiza ndoto yako au zako ni kubwa pia.
Chanzo:GPL
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.