Kamwe usikate tamaa, Hofu na Mashaka haviwezi kuwa jawabu la jambo lolote! - Napenda niwahakikishie maisha ya mtu huwa yalikwisha pangwa, hata pale waweza patwa na jambo baya, kupitia jambo hilohilo litazaa jambo jema, kwa sababu mambo mabaya hutuimarisha kupokea mambo mema. Tukumbuke hata watoto huzaliwa kwa uchungu na baada ya hapo huwa ni furaha kwa kupata mtoto. Pia hata mbegu za mimea ili ziote na kuzaa mazao mengi hufa na kuoza aridhini ndipo mimea mipya huzaliwa.
Katika maisha wakati fulani waweza fikwa na JAMBO lililo nje ya uwezo wako wa kulitatua.
NAKUSHAURI kuwa mtulivu na amini Mungu anajua jinsi atakavyotatua shida yako na kukupa majibu yafaayo, maana Mungu ni jawabu la mambo yote.
Ukiwa na hofu iliyopitiliza na kukumbuka shida hiyo saa zote NI KUJIBEBESHA MZIGO usioweza beba. Tusisahau uwezo wa binadamu wa kutenda una kikomo chake, na baada ya hapo Mungu peke yake ndo anaweza fanya ziada.
Katika mambo yako yote hakikisha unafanya sehemu yako unayomudu - yale usiomudu mwachie Mungu, kwa sababu ni dhahiri hatuwezi kuishi duniani kwa mafanikio bila kuwa na HAKIKA kuna mamlaka juu yetu yenye nguvu kuliko sisi na HIYO ndio tunayopaswa kuitumainia.
Jacob Noel Urasa
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.