ilipoishia
Nilirudi haraka kitandani baada ya kusikia simu yangu
ikinguruma, mawazo yangu yote nikijua lazima Lydia atakuwa amenijibu kitu,
mapigo ya moyo yakaanza kunienda kwa kasi maana jinsi ninavyompenda huyu mtoto
Mungu mwenyewe ndiye anayejua.
03.
Tofauti kabisa na nilivyofikiria ujumbe ule haukuwa wa Lydia
bali ulikuwa wa Tigo ukinikumbusha kulipa mkopo wa nipige tafu. Nilipochungulia
simu ya Lydia niliona bado ipo online halafu safari hii amebadilisha na picha
yake ya profile amemweka huyo bwana ake Boniface huku status yake ikosomeka:
wenye wivu wajinyonge; sijui alikuwa
akinilenga mimi?
Nilikasirika kwa kweli, safari hii nikazima taa na kujitupa
kitandani na kujikuta nikizama kwenye lindi la mawazo kuhusu maisha yangu kwa
ujumla, jinsi nilivyotoka kijijini na kuanza maisha ya kuhangaika mjini na
hatimaye kupata kazi ya kufagia kwenye kampuni maarufu ya Jambo Freight.
Mwanzoni nilikuwa nikiishi kwa shida sana kuanzia kula hadi
kulala lakini baada ya kuwekeza mishahara yangu ya miezi mitatu sasa na mimi
nimeweza kupanga na kuondokana na lawama za marafiki.
Lakini cha ajabu wakati mimi hayo nikiyaona ni mafanikio,
mpenzi wangu Lydia hayaoni kabisa na amedata kweli na muuza chipsi wa
Africasana, kwa kweli inauma lakini bado sijakata tamaa.
Nilishusha pumzi na kutazama vizuri chumba changu nilitazama
kuanzia paa lake ambalo lilionesha kuwa nyumba ile ni ya zamani maana mabati
yake yaliyochakaa yalishikiliwa na miti ya mtalawanda, nilipotazama kuta za
chumba kile nilishangaa kuona kikifanana kabisa na kile chumba nilichokiota
ndotoni.
Nilishtuka na kuanza kuutafuta ule ufa na lile shimo,
nililoliota, kweli niliuona na lile shimo dogo aliloingia yule panya mwanzoni,
nilistaajabu sana kwa hilo, nikarudi zangu kulala nikiwa na hofu huenda
nimeingia kwenye chumba cha mauzauza kama wanavyosimuliaga wenzangu.
Je, nini kitaendelea usikose kufuatilia..
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.