Wednesday, February 3, 2016

Published 2/03/2016 06:14:00 AM by with 0 comment

MAMA MKWE ANAMTAFUTIA MUME WANGU MWANAMKE MWINGINE!


Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 25, nimeolewa, naishi na mume wangu yapata miaka 3 sasa, tumebahatika kupata mtoto mmoja wa kike.

Wiki iliyopita mama mkwe alikuja nyumbani kumchukua mtoto wetu na kumpeleka kijijini kwao akidaia anakwenda kumuanzisha masomo awali. Mungu si Samatha nikasikia habari kutoka kwa ndugu zake wa karibu kuwa mama mkwe hakwenda kijijini kumuanzisha masomo mtoto wetu kama alivodaia awali bali kaenda kumtafutia mwanaye (mume wangu) mwanamke mwingine ili aachane na mimi.

Kumbe ndiyo maana hata mtoto aliamua kumchukua mapema ili atakaponiachanisha na mwanaye wabaki na mtoto wangu.

Kama ungekuwa ni wewe, au mimi ni dada, rafiki au jamaa yako ungenishauri nini? 
Na Timothi Mjuni:M&U
      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.