HOFU ni hali ya mtu au
kitu kuogopa kitu au jambo fulani, aidha kwa kuona labda yeye ni dhaifu kuliko
mtu mwingine au jambo husika au kwa kuhisi tu kuwa hawezi kufanya jambo fulani
lakini kumbe kiuhalisia angefanya na jambo lingefanikiwa.
Hofu ziko za aina nyingi
kuna, hofu ya kuzaliwa nayo, kurithishwa au kurithi au kutengenezewa.
HOFU YA KUTENGENEZWA
Hofu hii inaweza kuwa ni
ya kusikia, kuona au kusimuliwa kuwa jambo fulani ukilifanya huwezi kufanikiwa
kwa sababu ya kadha wa kadha kwa mfano:
Hofu yako inakuambia kuwa
huwezi kuwa kiongozi wa mtaa, kijiji, wilaya, mkoa, au taifa eti kwa sababu mzazi
wako hajawahi kuwa.
Kisa kwenye ukoo wenu
hakuna historia ya mtu kuwa kiongozi hivyo unaamini kuwa historia yako
inakuhukumu, inakuondolea sifa za kuwa kiongozi wa sehemu au jambo fulani.
Jambo ambalo halina ukweli
wowote, na kwa mtu mwenye kuthubutu hujaribu kuivunja roho hiyo (ya kuhisi kuwa
kwenye ukoo wenu hakujawahi kutokea mtu wa hivyo), ili kuifanya familia au ukoo
wake nao kuingia kwenye orodha ya viongozi ambao watakuwa wanatajwa na waoga
wengine.
Watu huamini mtu mwenye
mali au pesa nyingi labda ni mtu mwenye bahati zaidi kuliko wengine, wengine
huhisi labda mtu huyo ni mwema sana mbele za Mungu na ndiyo maana katunukiwa
mali hizo jambo ambalo si kweli kila kitu kinatafuta lakini cha kujifunza KUNA
WENGINE WANAPESA AMBAZO SI ZA HALALI WAMEWAUMIZA WENZAO ILI WAO WAWE NA PESA NA
WAHESHIMIKE.
Yawezekana ukoo au familia
yake haijawahi kufanya jambo fulani kubwa kiasi cha familia husika kupongezwa
na wanajamii wanaowazunguka.
Hii ni hofu mbaya, hofu
ambayo hata kama una elimu kubwa kiasi gani lakini bado inakutafuta na kuivunja
hofu hii ni kuwa na uthubutu wa ndani yako.
Hofu ya kuhisi wewe huna
nguvu ya kufanya jambo fulani, huwezi kwa sababu huna pesa, elimu, huna nguvu,
huna jina lolote wala heshima yoyote kwenye familia, ukoo au kijijini kwako
basi huwezi kufanya jambo hilo.
Usikose sehemu inayofuatia
ya mada hii…
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa