Ni simulizi nzuri
inayomhusu msichana mdogo anayeitwa Matrida, ambaye alipoteza wazazi wake wote
wawili, jambo lililopelekea kuanza kuishi katika mazingira magumu. Maisha
aliyoanza kuishi hakuwahi kuyafikiria kabla kwenye akili yake kama kuna siku
atakuja kuishi maisha hayo.
Matrida alianza kuishi
maisha ya shida sana tofauti na alivyokuwa akiishi na wazazi wake enzi za uhai
wao. Kutokana na ugumu wa maisha aliyokuwa anayapitia msichana Matrida alianza
kushawishika kwa kutafuta namna ya kuweza kuishi maisha ya furaha kama zamani
kiasi cha kufikia hatua ya kushawishika kuabudu MASHETANI ya ZIMAYA. Ni maswahibu gani
yaliyomkuta Matrida tangu alivyo jiunga na MASHETANI YA ZIMAYA.
Ilikua ni siku mpya kwa
upande wa Matrida, asubuhi na mapema baada ya kuamka mnamo majira ya saa 12:03
alfajiri alifungua mlango nakutoka chumbani kwake kuelekea sebuleni, wakati
huohuo baba na mama yake wakiwa usingizini.
Ni kawaida ya Matrida
kuwahi kuamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kuanza kufanya usafi wa nje pia
kuwasha jiko ili kuandaa kinywa cha siku hiyo kabla ya kuanza kufanya usafi wa
ndani.
Ilipofika saa 12:30,
Matrida alimaliza usafi wake wa nje na kubakiwa na usafi wa ndani, wakati
akijiandaa kuingia ndani, akiwa bado yupo mlangoni amekaa kwa uchovu wa kazi ya
siku hiyo akiwa anafikilia kufanya kazi iliyo baki lakini pale alipokaa kama
hatua tatu kuna kitu alikiona mbele yake.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U