Mimi ni binti
wa miaka
23 , huko awali niliwahi kuwa na uhusiano na kijana wa kwanza lakini
tukaachana na baadaye nikapata mwingine ambaye naye tuliachana.
Sijabahatika kupata mtoto, na niligundua wale
vijana wawili hawakuwa na mapenzi ya dhati na mimi zaidi ya kunichezea tu.
Baadaye nilipata
mpenzi ambaye niko naye hadi sasa ila tatizo ni mtu mzima ana miaka zaidi ya
hamsini.
Ninampenda sana
kiukweli kwa sababu sijawahi kupata au kukutana na mwanaume ambaye anajua kukea
na kujali kama huyu.
Nilimuuliza kama
ana mke akasema alikuwa na mkewe ana wana watoto wawili ila waliashaachana muda
mrefu na mwanamke yuko mkoani.
Changamoto ninayokutana
nayo ni way kunisema sana kuwa natembea na mwanaume mtu mzima ambaye siwezi
kufanya naye maisha ya baadaye.
Tatizo la pili,
huyu mpenzi wangu ana umbile doggo sana na tukishiriki mapenzi anakomea
mzunguko mmoja tu hwezi kuendelea au akijitutumua basi ni kwa shida sana.
Lakini pia
nimekuwa nikiambiwa kuwa huyu mzee ni Malaya sana lakini najiuliza umalaya
anaufanyaje wakati hawezi kumridhisha mwanamke au kushiriki tendo kwa mizunguko
mingi zaidi.
Niko njia panda
sana kuhusu mpenzi wangu, ila nampenda sana, nawaogopa vijana kwani wao wako tayari kukuchezea na si
kukuoa.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U