NILIPOISHIA...
Nilifanikiwa kukutana na jamaa mmoja ambaye alikuwa ni
dereva na kuniahidi kunisaidia kuhusu tatizo la mwanangu.
SONGA NAMI...
Mwili ulikuwa umepooza sana kwa sababu ya mawazo,
akili ikiwa haifanyi kazi vizuri, usoni ukiniangalia unajua kabisa kuwa huyu
mtu ana matatizo makubwa na anahitaji msaada wa hali na mali.
Muonekano wangu wa kinyonge, uchovu, na mawazo
niliyokuwa nayo ndiyo iliyomfanya yule dereva anionee huruma na kutaka
kunisaidia.
Nilikubaliana naye na tukawa karibu sana, baada ya muda aliniomba twende akanisaidie
kwenye Hospitali ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. Kwa kuwa nilitaka mtoto wangu
apone tatizo lake la mguu hivyo nilikubaliana naye. Tulisafiri hadi Moshi ambapo akachukua chumba
akawa anakuja kunisalimia na kuondoka,
mwisho wa siku jamaa akanitolea uvivu na kutaka penzi nilikataa lakini
jamaa akaendelea kulazimisha.
Alivyoona kuwa sitaki jamaa akaniachia pesa kisha
akawa haji kunitazama na wala ishu ya kumpeleka mtoto wangu hospitali hakuwa anaizungumzia
tena.
Nilijaribu kumigia simu na kumkumbusha kuhusu
alichoniahidi lakini hakawa haelewekieleweki.
Nilikaa gesti kwa wiki moja huku jamaa akiwa aonekani.
Nini kilifuatia baada ya kukaa wiki nzima bila
msamalia mwema ambaye alitegemea kumsaidia leo anataka apewe penzi.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba,
Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na
M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U