Ningependa kupata ushauri wenu, ni miezi kadhaa tangu rafiki yangu
kipenzi afunge ndoa na mchumba wake wa muda mrefu.
Ila tangu siku ile ya kwanza kunipeleka kwake mkewe, (mai shemela) amekuwa
akinishirikisha mambo yake mengi ya siri kuliko mumewe.
Siku moja alikuja nyumbani, nilimkaribisha kama shemela lakini
nilishangaa kuona ananitaka kimapenzi!
Nilimkatalia lakini tangu siku hiyo nikienda kwake ananiambia kuna siku
atafanya jambo la chochote ili mimi niwe
naye..
Nipo kwenye wakati mgumu, naomba ushauri wenu, je, nikimwambia rafiki
yangu atanielewa au ndiyo nitaonekana Hasidi na kuvuruga ndoa yake?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba,
Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na
M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U