Shikamoo kaka.!! Bro G, asante kwa ushauri wako kupitia Gazeti
la Ijumaa Wikienda.
Naomba ushauri wako tafadhali, mimi ni binti wa miaka
20 nina muhusiano ya kimapenzi na mkaka mmoja ana miaka 27.
Ninampenda sana nay eye ananipenda, ameishanitolea
barua ya uchumba na hivi karibuni anataka kunioa.
Nimkutana faragha na mchumba wangu kama mara mbili
nilichokiikuta ndicho hasa kimenifanya niombe ushauri wako.
Eti mchumba wangu kwa umri alio nao hajatahiriwa,
nimeumia na kufedheheka sana.
Sijawahi kumwambia mtu mwingine zaidi yako, na hata
yeye mwenyewe sijaonyesha dalili zozote kuwa nimefahamu hilo.
Ila naumia sana kuhusu kutokutahiliwa kwake, najiuliza
nifanyaje na mimi nampenda mchumba wangu.
Mtu yeyote unayesoma ushauri huu, naomba maoni yako
kwani nahisi kuchanganyikiwa, kuona karne hii bado kuna watu hawajatahiriwa.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U