Nilizaliwa miaka ya 70 nikiwa mzima wa afya njema na nikafanikiwa kupata mwenzangu ambaye nilimpenda sana na yeye alinipenda.
Nashukuru Mungu alinijalia nikapata watoto 6 kwa mwanamke ambaye
nilikuwa naishi naye kama mke wangu. Maisha yalisonga kama kawaida huki
changamoto za hapa na pale zikitokea katika maisha yangu na familia yangu.
Muda
wote huo nilikuwa naishi katika mkoa wetu nikiwa na familia yangu. Ila mwaka
1990 kwangu uligeuka mwaka wa machungu sana katoka maisha yangu. Na ndiyo maana
hata wewe mwana M&U nimeamua kusimulia ili uweze kujifunza kuwa USIONE
VYAELEA VIMEUNDWA!
Je, ni nini hivyo basi usikose wiki
ijayo kwenye mkasa huu wa kweli. Unaomsumbua Majuto.
Kwani baada ya kuokota ile hela
nilianza kuugua sana na kupelekea kupooza kwa sehemu kubwa ya mwili wangu.
Nilifanikiwa kwenda kwenye hospital
za eneo nililokuwepo lakini sikupata nafuu. Nilihama makazi kutoka sehemu
niliyokuwepo na kuhamia wilayani lakino bado huduma ya kunifanya nirudie hali
yangu ilishindikana.
Nilishauriwa niende Hospitali ya Rufaa ya Bugando
jijini Mwanza, tatizo langu ni ukosefu wa pesa kwani maisha yangu ni duni sana,
naishi kwa kuombaomba nikiwa nimekaa kwenye kiti cha magurudumu huku mtoto wangu
mmoja akinitembeza mitaani.
Baada ya miaka kupita mke wangu
alipoona siponi aliamua kunitoroka na kuniacha mimi na watoto wangu. Napenda
kuwaomba Watanzania waweze kunisaidia kwa namna yoyote ile niweze kupata
matibabu pia kunisomeshea watoto wangu.
Sikupenda kuwa hivi nilivyo ila
Shilingi 10 niliyoiokota ndiyo imefanya mateso makubwa sana kwangu. Najua
umekuwa ukihisi kuwa una matatizo sana yanayokukabili lakini tatizo lako na
langu lipi kubwa? Kama ni langu kwa nini ukate tamaa wakati mimi bado
najitahidi kupigana ili nipote na ndiyo maana nimepata nafasi ya kuzungumza
nawe wana M&U.
Kama una mkasa, ushauri, au simulizi
yoyote ya mapenzi unaweza kuniibox. Jiunge na M&U WhatsApp, M&U SMS au
M&U kwenye group la Faceboo KUPATA HABARI ZA MAPENZI KILA SIKU.
Pia usikose kutembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au like ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao
wa Kijamii wa Facebook.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.