Sunday, September 11, 2016

Published 9/11/2016 12:00:00 PM by with 0 comment

ULIMWENGU WA WENDAWAZIMU-04

Na M&U


Ilipoishia…

Wakati akiendelea kuwaza na kuwazua hili na lile, anakumbuka miaka kadhaa ambapo serikali ya Marekani ilipokuwa ikihangaishwa na gaidi hatari, Osama bin Laden. Anakumbuka ni yeye pamoja na huyu Christopher Marwa ndio waliofanikisha kubaini ni sehemu gani alipokuwa kajificha gaidi huyo.

Endelea…

Anaikumbuka pia kazi nzuri aliyoifanya Marwa wakati Tanzania ilipotuma majasusi wake nchini Kongo na kuweza kubaini kambi kubwa ya waasi iliyokuwa katikati ya misitu ya nchi hiyo. Hivyo basi kutokana na shughuli hizo, aliweza kuaminiwa na kisha kupewa ukuu wa kitengo cha mawasiliano ndani ya ikulu.

Mbelike kama jasusi hakupaswa kuogopa chochote kwani alikuwa fiti mno kila idara, lakini kumpeleleza Christopher ilikuwa ni habari nyingine.

Aliiangalia saa yake ya mkononi na kubaini kuwa tayari ilikwishatimia saa mbili za usiku hivyo aliona ndio muda mwafaka wa kuianza kazi yake. Hivyo aliichukua bastola yake na kuichomeka kwenye suruali yake ya jinzi na kisha alifunga mlango na kuchukuwa usafiri hadi New Africa Hotel.
       ****
"Leila chukua teksi haraka sana uelekee New Africa Hotel. Uhakikishe unafanya kazi takatifu, na uwe makini sana. Sawa!"

"Sawa bosi." Leila aliitika kwa heshima wakati alipokuwa akiongea na bosi wake kwenye simu. Alijiandaa haraka na kisha kujiremba, alivaa mavazi yake ambayo siku zote aliamini yalimpendeza sana. Kwa jinsi alivyokuwa amebarikiwa umbo zuri la kike pamoja na sura ya kuvutia, hakika alipendeza mno. Alikuwa kavaa nguo ambazo ziliacha baadhi ya sehemu za mwili wake kuonekana na kuwatamanisha vidume vikwale visivyopitwa na aina hiyo ya wadada.

Taratibu baada ya kuingia hotelini hapo, Leila kwa mwendo wa madaha alitafuta sehemu iliyokuwa imetulia na kukaa huku kila jicho la vidume waliokuwa eneo hilo likipata burudani ya karne.


Je, nini kitaendelea? Fuatana nami sehemu ijayo.

Kwa USHAURI, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI, HADITHI, MACHOMBEZO, USHUHUDA NA UJASIRIAMALI Jiunge na M&U WhatsApp kwa Na 0657486745 kwa MADA ZA KILA SIKU.
Pia tembelea https://www.facebook.com/mimi-na-uhusiano-1584071311866497/… au https://www.instagram.com/mimi_na_uhusiano au www.miminauhusiano.blogspoti.com
      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.