Monday, September 26, 2016

Published 9/26/2016 12:27:00 PM by with 0 comment

USHAURI WAKO

MUME WANGU HALALI NDANI NAPOKUWA KAZINI!

Mimi ni mama wa familia ninaishi na mume pamoja na watoto wangu. Kutokana na majukumu ya kazi zangu kuna wakati nabadilisha zamu na kuingia usiku.

Lakini nilikuja kuhisi kuwa mume wangu amekuwa halali ndani pindi ninapokuwa zamu ya usiku, nikaamua kuweka mtego ili nijiridhishe:

MTEGO WA KITANDANI 
Nilipoingia zamu ya usiku nikaweka mtego kwa kutandika kitanda kwa mtindo flani ili kama hatolala nijue, kweli mtego ule ulinasa, wangu hakulala nyumbani.

MTEGO WA SABUNI   Mtego mwingine niliweka sabuni mpya bafuni ili kama akiamka si lazima ataoga lakini na yeyewe nikaikuta iko vilevile.

MTEGO WA UMEME  kuna siku nilinunua unity chache za umeme ili ikifika muda flani uzimike, kweli ukazimika usiku kesho yake nikamuuliza nasikia umeme jana usiku ulikatika akasema yeye hafahamu labda kama ulikatika usiku sana. Akasema yeye alirudi nyumbani saa 3 usiku akaingia kulala kwahiyo hakujua kitu.

Wakati huo dereva wetu wa boda×2 anadai hiyo saa 3 ya usiku anayosema alimuita sehemu akachukua pesa nakuondoka.

Hapa nilipo nina maumivu sana na kitendo cha mume wangu, nimejiridhisha je, nichukie hatua zipi?

      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.