Mkuu po le sana na kazi, nafuatilia sana elimu na ushauri wako
kuhusu mahusiano. Mimi ni mwanaume wa miaka 48, nilianza maisha ya kujitegemea
nikiwa na miaka 25, katika mishemishe na maisha yangu yote hasa ya mapenzi
sikubahatika kupata mke wa kweli.
Wengi wao walikuwa ni pasua kichwa tu nilibahatika kupata watoto 2
kwa wanawake wawili tofauti. Mtoto wangu wa kwanza anasoma kidato cha pili na
wa pili anasoma darasa la pili, wote wako kwa mama zao.
Naweza kusema kwa sasa mimi ni mtu mzima kutokana na umri wangu
(miaka 48)cha ajabu eti ndiyo anatokea kabisa mwanamke wa ndoto zangu ina yeye
ana miaka 32, ni mvumilivu, ananipenda, ana bidi ya maisha n ahata mimi nampenda
sana.
Dukuduku langu ni kuwa kwa mimi kupishana na mchumba wangu miaka
16 huoni kama nitalaumiwa na jamii kuwa nimeoa mtoto mdogo, lakini vipi kuhusu
suala mapenzi hawezi kufika sehemu akaanza ujanja ujanja kwa kuwa nitakuwa
namzidi umri sana.
Kwa USHAURI, MIKASA YA
KWELI YA MAPENZI, HADITHI, MACHOMBEZO, USHUHUDA NA UJASIRIAMALI Jiunge na
M&U WhatsApp kwa Na 0657486745 kwa MADA ZA KILA SIKU.
Pia tembelea https://www.facebook.com/mimi-na-uhusiano-1584071311866497/… au https://www.instagram.com/mimi_na_uhusianoau www.miminauhusiano.blogspoti.com
Pia tembelea https://www.facebook.com/mimi-na-uhusiano-1584071311866497/… au https://www.instagram.com/mimi_na_uhusianoau www.miminauhusiano.blogspoti.com
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.