Thursday, September 8, 2016

Published 9/08/2016 11:00:00 AM by with 0 comment

USHAURI WAKO:MWALIMU WANGU ANANITAKA KIMAPENZI


Mimi ni msichana wa miaka 26, niliamua kujifunza ufundi wa kushona nguo ili niweze kujikimu na maisha yangu, nilipata sehemu kwa fundi mmoja ambaye ni mkaka na ana familia yake.


Baada ya kumaliza mafunzo yangu yule kaka ambaye ni fundi wangu aliniambia kwa kuwa sijapata mtaji basi niendelee kukaa kwenye ofisi yake wakati nikitafuta mtaji.


Nilikubaliana naye na nikaanza kupiga kazi kama kawaida lakini baada ya muda akaanza kunitongoza , nimemkatalia na kumwambia kuwa nina mchumba wangu lakini anaendelea kunisumbua sana imeshakuwa mpaka usumbufu sana, nafika sehemu nachukia hata kwenda kazini na wakati mwingine nawaza au nimwambie mkwe?


Naomba maoni na ushauri wako tafadhali kama ungekuwa wewe ungefanya nini?

Kwa USHAURI, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI, HADITHI, MACHOMBEZO, USHUHUDA NA UJASIRIAMALI Jiunge na M&U WhatsApp kwa Na 0657486745 kwa MADA ZA KILA SIKU.
Pia tembelea https://www.facebook.com/mimi-na-uhusiano-1584071311866497/… auhttps://www.instagram.com/mimi_na_uhusiano au www.miminauhusiano.blogspoti.com

      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.