Nimshukuru MUNGU kwa kila jambo linaloendelea chini ya jua
dhidi yangu na wewe, kwani nina amini kabisa kuwa maisha yote unayoyapitia
tayari yameishaandikwa kwenye kitabu chako, kinachofanyika ni kurasa za kitabu
chako kufunguka kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa mwisho.
NILIKUPENDA MPENZI
WANGU LAKINI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI YANGU, yawezekana wewe naye ni miongoni mwa
mwanadamu ambaye umewahi kujikuta ukitamka maneno hayo kwa sababu ya ndugu,
jamaa, rafiki, mpenzi, mke au mume, wazazi wako au mtoto wako kufariki dunia.
Basi pata
muda mchache wa kumkumbuka au kuwakumbuka wapendwa wako ambao wamekwisha
tangulia mbele ya haki, lakini pia na wewe jiombee kwa kuimaliza salama siku ya
leo.
Hakuna jambo
ambalo huwaumiza na kuwasumbua sana wanadamu kama kifo, hiki ndicho kitu pekee
duniani ambacho huifanya akili ya mwanadamu kufikiri zaidi ingawa pamoja na
kufikiria kote huko mhusika ushindwa kupata muafaka wa alichofikiria na kuamua
kuacha tu na kujisemea moyoni MWACHE MUNGU AITWE MUNGU.
Kila
mwanadamu huwa kwenye kipindi kigumu sana hasa anapoondokewa na kipenzi chake
bila kujali ni mpenzi, mchumba, ndugu, jamaa, rafiki, mlezi au mzazi. Inauma sana,
msiba usikie kwa jirani yako lakini usikupate ingawa kila mmoja wetu utampata.
Kifo kinaumiza,
kinasikitisha na kuhuzunisha sana, kwani mtu ambaye ulimpenda, ulimtegemea,
ulimshauri au alikushauri, msaada kwako wa hali na mali, ulimpenda na
akakupenda lakini leo unaamka huko naye ila ghafla unaambiwa au unamuona akiwa
hazungumzi, hacheki, hatabasamu tena kama zamani, hali, hatembei, hataniani
nawe kama zamani.
Ni mwili
pekee yake ambao unauona lakini nafsi yake haina uhai, na kamwe hautamuona tena maishani mwako, saa kadhaa
zijazo mara atakapopelekwa kwenye nyumba yake ya milele. Inauma, kibinadamu.
Nafsi ya
mhusika hubaki ikiwa haina amani tena, haioni raha ya kuishi dunia wakati
kipenzi chake kishaaga dunia, hujiona kama mtu ambaye amekosea sana na pengine
amenyang’anywa kitu muhimu sana katika maisha yake. Lakini ukweli ni kwamba
mweza wako ulimpenda lakini MUNGU kampenda zaidi na ndiyo maana kamtwaa.
Bila shaka
kila mwanadamu anatamani kuiona pepo ila wengi wao uogopa kufa na husahau kuwa
hakuna njia nyingine ya kuweza kuiona pepo isipokuwa kufariki dunia.
Ndugu yangu
mwanaM&U kikubwa ni kuangalia mapito yetu na kujirekebisha kwa kufanya yale
yote yampendezayo Mungu.
Najua wanadamu tumeumbwa kusahau na kupotezea lakini
tunapaswa tufahamu kuwa kifo hakina hodi, siku, saa wala dakika. Hakina maandalizi
yoyote bali unachopaswa ni kujiandaa muda wowote kuwa muda ukifika basi MUNGU
AIPOKEE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI.
Na:M&U
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.