Na M&U
Ilipoishia…
Taratibu baada ya kuingia hotelini hapo, Leila kwa mwendo
wa madaha alitafuta sehemu iliyokuwa imetulia na kukaa huku kila jicho la
vidume waliokuwa eneo hilo likipata burudani ya karne.
Songa nayo…
Alishusha pumzi ndefu huku akiangaza huku na kule kama
kibaka mkwapuaji. Alikisogelea kitasa cha mlango na kuusukuma na kisha kuzama
ndani. Alimkuta mke wake akiwa amejikunyata huku machozi yakimtoka, hakuweza
kuelewa ni sababu ipi iliyomfanya mke wake kuwa katika hali hiyo.
Alimsogelea akamshika mkono na kisha kumkumbatia, hali
iliyosababisha mke wake azidi kupata hasira na mwishowe alianza upya kilio huku
akijaribu kujinasua kutoka mikononi mwa mume wake.
"Mume wangu ulikuwa unaongea na nani kwenye
simu?"
"Nilikuwa naongea na mkuu wangu wa kazi."
Alijibu Christopher huku akiyakwepesha macho yake yasigongane na ya mkewe Rynah
kwa uongo aliousema.
"No Chris unanidanganya, ulikuwa ukiongea na wanawake
zako huko halafu unaniambia eti ulikuwa unaongea na mkuu wako kweli! Hivi
unanifanya mimi mjinga siyo! Sasa leo nataka talaka yangu, halafu ubaki na hao
akina Leila wako." Aliongea kwa masikitiko mno Rynah huku machozi
yakiulowanisha uso wake. Macho yalimvimba kwa kulia sana huku akimlaani mumewe
kwa kutokumjali.
Ndoa yao ilitiwa misukosuko mara tu baada ya Christopher
kujiingiza kwenye kundi la wafanyabiashara wa dawa za kulevya, ambao
walimshawishi ili iwe rahisi kwao kupata taarifa zilizokuwa zikiendelea ikulu
juu ya operesheni aliyoianzisha rais, ya kuhakikisha anadhibiti biashara hiyo
haramu.
Christopher aliahidiwa donge nono na wazito hao endapo tu
atakubali kuwa chini yao. Maadili ya kazi yake yalimbana mno, na kibaya zaidi ni sehemu nyeti aliyokuwepo
ya ukuu wa mawasiliano ya ikulu. Hivyo kukubali kwake kuwa chini ya wazito hao
ilikuwa sawa na kuuza ramani ya nchi yake.
Alijaribu kukataa dili hilo, lakini mwisho wa siku
alikubali, na huo ukawa mwanzo wa kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.
Mwanzoni wakati ameteuliwa kushika wadhifa huo, alikuwa mtiifu na mwaminifu
mno, lakini baadaye pesa ikamfanya kuwa msaliti wa nchi yake.
Nini kilifuatia,
tukutane sehemu inayofuatia…
Kwa USHAURI, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI,
HADITHI, MACHOMBEZO, USHUHUDA NA UJASIRIAMALI Jiunge na M&U WhatsApp kwa Na
0657486745 kwa MADA ZA KILA SIKU.
Pia tembelea https://www.facebook.com/mimi-na-uhusiano-1584071311866497/… au https://www.instagram.com/mimi_na_uhusiano au www.miminauhusiano.blogspoti.com
Pia tembelea https://www.facebook.com/mimi-na-uhusiano-1584071311866497/… au https://www.instagram.com/mimi_na_uhusiano au www.miminauhusiano.blogspoti.com
@@@@
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.