Asante Mungu kwa siku
nyingine tena nakutana na ndugu zangu ambao bila shaka wewe Jalali ulifanya
hivyo ulivyofanya na kutukutanisha sisi kama ndugu, jamaa marafiki ambao
tunaweza kusaidiana pale inapobidi.
Nimshukuru kila
mwanaM&U aliyeko mkoa wowote ule nchinI Tanzania.
Jiamini kuwa wewe ni mtu
muhimu sana kwangu na kwa jamii nzima kwa sababu tu unajitambua na kuamua
kutafuta suluhu ya matatizo yanayokusibu.
Somo la leo linazungumzia sana kuhusu baadhi ya
wapenzi ambao wanashindwa kutumia vizuri miili ya wapenzi wao haswa
wanapokabidhiwa wakati wa faragha.
Mapenzi ni ufundi, ni
lazima ujue kucheza na hisia za mwenza wako, ujue ni viungo vipi ambavyo akipapaswa
uhisi raha, ni kiungo kipi akikunwakunwa anahisi utamu ni sehemu ipi ya mwili
wake akifinywafinywa anasikia hamu.
Nilichojifunza baadhi ya
wapenzi hawajui kuwatumia wapenzi wao wanakuwa nao faragha kwanza wanakuwa
wanwabana sana na kuwafanya wanshindwa kupata raha stahiki wakati mwingine mpe
huru afanye anachopenda .
Unakuta mpenzi wako
anapenda sana kujituma na kujishugulisha anapokuwa faragha lakini mwenzake
anakuwa mzembe mzembe anakuwa mtu mwenye aibu jambo linalofanya kumkata stimu
mwenzako.
Hilo ni kosa na tatizo
sana kwenye uhusiano kama mwenziyo unaona yuko juu basi hakikisha na wewe
unajitahidi kumpandilia huko huko ili mkutane
lakini ukizembea mwenziyo yuko juu wewe unashuka china bila shaka
utakuwa umeharibu sana mechi ya siku hiyo.
Itaonekana hakuna
ushindani wa kutosha ni kama timu moja ni kubwa na ina nguvu lakini nyingine ni
dhaifu isiyojiweza, kwa tabia hiyo unakosa vitu vingi sana unapokuwa faragha na
mpenzi wako. Mpe ruhusa au mruhusu akufanyie manjonjo anayoyataka na yale
ambayo anapenda kufanyiwa
Kutokumpa nafasi mpenzi
wako kutamafanya atamani kuchepuka na akikutana na mtaalamuna basi ujue kabisa
kuwa penzi lako litakuwa limepata ufa.
Hivyo jaribu
kushirikiana na mwenza wako kwa kumuuliza nini anakipenda kwenye mapenzi,
mtengee mwili wako auchezee na kuutawala ilivyo panapostahili.
Ni hakika kama una
mwenza wako unaweza kuanza majaribio leo kwa kufanya kwa vitendo kwa wewe
ambaye hujaoa au kuolewa tafadhali usiafnye UZINZI.
Niwakumbushe wale wote
ambao wako tayari kuchangia mchango wa uanzishwaji wa M&U kama taasisi na
tupigane kufika lengo letu la kuanzisha chuo chetu cha ushonaji. Hivyo
nakukumbusha kuchangia ule mchango wa kiingilio na ada , asanteni kwa wale
ambao wamejitoa MUNGU ATUSIMAMIE KWANI INAWEZEKANA.
Na:M&U
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.