Wednesday, September 7, 2016

Published 9/07/2016 04:09:00 PM by with 0 comment

ULIMWENGU WA WENDAWAZIMU-01

Na. M&U
Ndege ya shirika la ndege la Marekani, United Airlines ilizidi kuyakata mawingu ikitokea Tanzania kuelekea Marekani huku ikipita katika viwanja vya ndege vya nchi za Kenya, Afrika Kusini, Uholanzi kabla haijatua Los Angels, nchini Marekani.


Katika kiti cha nyuma kabisa ndani ya ndege hiyo alikuwa amekaa mtu mmoja hatari mno duniani, jasusi kutoka Tanzania, Mbelike Mbonde. Alikuwa akielekea nchini Marekani kwa kazi maalum aliyokuwa ametumwa na rais wa nchi yake pamoja na idara ya upelelezi ya nchi hiyo.
Hakuwa na papara hata kidogo, zaidi ya kuendelea kuburudika na mziki uliokuwa ukimliwaza vya kutosha, huku akiwaza ni namna gani ataweza kufanikisha kazi aliyokuwa katumwa na nchi yake.


"Those passengers land at Jomo Kenyata airport please get prepare, because we are about few minutes to reach there."(Abiria wote mnaoshukia uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata, jiandaeni, kwa sababu tuna dakika chache kuweza kutua hapo).

Ilikuwa ni sauti ya mhudumu wa kike wa ndege hiyo iliyokuwa ikisikika kwa lugha kadhaa, ikiwapa taarifa abiria  waliokuwa wakihitimisha safari zao nchini Kenya na pia ikiwakumbusha abiria wote kufunga mikanda.
Baada ya tangazo hilo kusikika, haukupita muda mrefu ambapo ndege hiyo kubwa na ya kisasa iliweza kuinama kwa mbele na baadaye matairi yake madogo yaligusa ardhi, na kuanza kuserereka kwa kasi na kisha kusimama kando ya jengo kubwa uwanjani hapo.

Wale abiria waliokuwa wakishukia nchini humo waliteremka, huku wale waliokuwa wakiendelea na safari yao wakibaki ndani, kwani ilikuwa na muda mchache kabla ya kuruka tena.
Wakati zikiwa zimebaki dakika kumi na tano kabla ya ndege hiyo kuruka tena, Mbelike anastukia simu yake maalumu ya kijasusi ikiita kwenye saa yake ya mkononi. Alipoiangalia anashangaa ikiwa inatoka ikulu ya Tanzania.
Je, nini kitatokea? Tukutane kesho.  


USIKOSE HADITHI HII KILA SIKU MCHANA KWA KUJIUNGA NA M&U WHATSAPP KWA NAMBA 0657486745. Kwa USHAURI, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI, HADITHI, MACHOMBEZO, USHUHUDA NA UJASIRIAMALI Pia tembelea https://www.facebook.com/mimi-na-uhusiano-1584071311866497/…au https://www.instagram.com/mimi_na_uhusianoau www.miminauhusiano.blogspoti.com
      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.