Mimi ni mama mjane ambaye mume wangu
alifariki dunia takribani miaka 3 iliyopita kwa tatizo la mshtuko wa moyo. Ni mama
wa miaka 42 na nina watoto wanne.
Nimekuwa nikiishi katika upweke kwa
muda mrefu sana na hata nilipoppata mtu wa kunifariji hakuwa na mapenzi ya
kweli zaidi ya kunitumia na kuchikichia na kunifanya niendelee kutamani na
kukumbuka uwepo wa marehemu mume wangu.
Baada ya kukaa kwa muda mrefu nikiwa
na upweke wangu hatimaye nimempata kijana wa miaka 33 ambaye yuko nje ya nchi. Ananipenda
sana na mimi ninampenda na yuko tayari kuishi na mimi, ameshanitumia baadhi ya
pesa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa Bongo na hata pesa ya matumizi amekuwa
akinipatia.
Nilimuuliza kwa nini ameamua kuwa na
uhusiano na mimi mtu mzima ambaye ninamzidi miaka 9, alisema kuwa utu uzima
siyo tatizo kwake ni dawa kwani anaamini kuwa mabinti hawana uchungu na maisha
hawawezi kutunza na kuendeleza mali zake ambazo zipo hapa nchini.
Kiukweli nampenda lakini wasiwasi
wangu ni utofauti wa miaka yetu naona kama jamii itanishangaa na kunisema sana.
Kama mfuatilia wa makala za M&U
naomba ushauri wenu ili niweze kujua nini cha kufanya.
Kwa
ushauri, mikasa ya kweli ya mapenzi, hadithi, machombezo, ushuhuda na
ujasiriliama na Jiunge na M&U WhatsApp, M&U SMS na M&U Facebook
group kwa Na.0657486745 kupata makala za mapenzi zenye mafunzo kila siku.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.