Mimi ni msichana wa miaka 25 ni Mkristo ila mpenzi wangu ni Muislamu
tumejaliwa Kupata mtoto mmoja.
Mpaka sasa tuna miaka 7 kwenye mahusiano yetu, toka nipate
ujauzito baba yangu mzazi amekua mkali sana kwa sababu tu nimezaa na mtu wa imani
nyingine, hivyo hakutaka kumfahamu mzazi mwenzangu wala ndugu zake kibaya zaidi
kasema kama sitamsikiliza basi ataniachia laana na hatonisomesha chuo.
Ilibidi niwe mpole, nikamsikiliza nikasoma na nikafanikiwa kupata
digrii, lakini muda wote amekuwa akiniuliza kama bado nina uhusiano na huyo
mzazi mwenzangu nikamdanganya lakini ukweli ni kwamba mpaka sasa ninaishi naye.
Naweza kusema tunapenda sana na Mungu ametukutanisha kwani
tumeshibana na tunaelewana ila baadhi ya dada, mama na ndugu zangu wanafahamu
kuwa naishi na jamaa.
Baada ya miezi kadhaa kupita mpenzi wangu ameniambia yupo tayari
kunioa rasmi na ndugu wote wajue uhusiano wetu, kwani upande wa mpenzi wangu
wamefurahi na kunipokea.
Mchumba wangu ameniambia hawezi kunilazimisha kuhusu kubadili dini
ni maamuzi yangu na wala ndugu zake hawana mamlaka ya kufanya hivyo.
Nilijaribu kumshirikisha kaka yangu mkubwa akakubaliana na mimi na
kusema amefurahi kuona nimepata mume wa kunioa na yuko tayari kunisaidia tatizo
ni baba yangu kwani ni mtu wa kutoa laana mpaka sasa kuna ndugu zangu wawili
aliwahi kuwapa maneno makali na hawana maisha mazuri.
Mtoto wangu yuko nyumbani kwetu lakini baba amepiga marufuku
asichukulie hapo na hata kama baba atafariki dunia mtoto wangu asitoke
pale.Naumia sana moyoni mwangu.
Hivi ni dhambi kwa Mkristo kuolewa na Muislamu na kila mtu kubaki
na dini yake?
Kwa USHAURI, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI,
HADITHI, MACHOMBEZO, USHUHUDA NA UJASIRIAMALI Jiunge na M&U WhatsApp kwa Na
0657486745 kwa MADA ZA KILA SIKU.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.