Friday, September 9, 2016

Published 9/09/2016 12:00:00 PM by with 0 comment

ULIMWENGU WA WENDAWAZIMU-03

Na M&U

Ilipoishia….
Aliongoza hadi chumbani humo na kumkuta bwana Kembo akiwa na watu wengine watano ambao hakuwatambua pamoja na mheshimiwa rais. Hakushtuka sana kuwaona watu hao ndani ya chumba hicho ambacho ni nadra sana kutumika, ila hofu iliyomwingia ni juu ya wito wa ghafla kiasi hicho.

Songa nayo…

"Tumeamua kukatisha safari yako ya Marekani kwa sababu ambazo tumeona unafaa kuzitekeleza kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa. Wewe ni mtu muhimu sana katika idara yetu ya kijasusi, hivyo tunakupa majukumu mazito la kuhakikisha unafanikiwa. 

Ndani ya serikali hii na hasa kwenye idara yetu kuna watu wanavujisha siri zetu na za nchi yetu, vile vile watu hao wanashirikiana na wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya ili kuhakikisha hatufanikiwi katika mipango yetu ya kuwafikisha mbele ya sheria. Sasa basi kitu unachopaswa kufanya ni kufuatilia nyendo za huyu mkuu wa mawasiliano wa hapa ikulu, bwana Christopher Marwa, kwa maana tuna wasiwasi nae ingawa hatuna uthibitisho. 

Hii kazi unatakiwa kuifanya kuanzia sasa. Taifa linakutegemea!" Aliongea na kuhitimisha mkuu huyo wa shirika la kijasusi nchini. Hapakuwa na muda wa kupoteza, Mbelike alitoka katika chumba hicho na kisha kuelekea kwake kujipanga kutekeleza kazi aliyopewa.

Alifika kwake akachukuwa taulo lake na kisha kuingia bafuni kuoga ili kuondoa uchovu na kuiruhusu akili yake kutafakari kipi cha kufanya ili kutekeleza agizo hilo.

Alipomaliza kuoga alijibwaga kitandani na kuanza kuwaza mambo kadhaa hasa kazi nzito iliyokuwa mbele yake.
"Mmh! Kumpeleleza mtu kama Christopher, yataka ujasiri wa kujitoa mhanga." Alikuwa na haki ya kuwaza vile kwa sababu mtu aliyepewa kumfuatilia nyendo zake hakuwa mtu wa mzaha hata kidogo, na kibaya zaidi anamjua vizuri mno.

Wakati akiendelea kuwaza na kuwazua hili na lile, anakumbuka miaka kadhaa ambapo serikali ya Marekani ilipokuwa ikihangaishwa na gaidi hatari, Osama bin Laden. Anakumbuka ni yeye pamoja na huyu Christopher Marwa ndio waliofanikisha kubaini ni sehemu gani alipokuwa kajificha gaidi huyo.

Je, ataweza kumchunguza Christopher mtu hatari kama yeye?

Usikose kesho, muda kama huu.
Kwa USHAURI, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI, HADITHI, MACHOMBEZO, USHUHUDA NA UJASIRIAMALI Jiunge na M&U WhatsApp kwa Na 0657486745 kwa MADA ZA KILA SIKU.
Pia tembelea https://www.facebook.com/mimi-na-uhusiano-1584071311866497/… au https://www.instagram.com/mimi_na_uhusiano au www.miminauhusiano.blogspoti.com

@@@
      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.