USHAURI WAKO:
MUME WANGU ATAKI NIKASALIMIE KWETU
Nashukuru Mungu kwa kunipa mume mwema ila kweli nimeamini kuwa kila binadamu ana mapungufu yake, pamoja na mume wangu kunipenda na kunijali vivyo hivyo mimi.
Lakini kina ninapomwambia mume wangu kuwa naomba nisafiri ili nikawasalimu ndugu zangu ana kataa na kugeuka mbogo.
Basi ndani hakukaliki hata kwa siku mbili analizungumzia suala hilo na kusafiri. Cha ajabu yeye anasafiri na nikimwambia mbona yeye huwa anasafiri?
Ananiambia yeye ni mwanaume na ni baba mwenye nyumba sipaswi kushindana naye.
Kiukweli hizi ndoa ni ndoano, zina mambo makubwa sana. Kwa hiyo inakuwa kama niliolewa ili nitenganishwe na ndugu zangu!
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.