Monday, August 22, 2016

Published 8/22/2016 10:00:00 AM by with 0 comment

MDOGO WAKO WA DAMU ANAPOHARIBU NDOA YAKO!

Kiukweli inauma sana hasa unapogundua kuwa mumeo ambaye unampenda na kumuheshimu leo anatembea na mdogo wako wa damu.
Yamenikuta ndiyo maana najaribu kukushirikisha wewe mdau wa M&U ili niweze kupta ushauri wangu. Mimi ni mwanamke mwenye watoto 2 ninaishi na mume wangu mwaka wa 10 sasa, hivci karibuni mdogo wangu wa kike alikuja kunitembelea nikamkaribisha ingawa tabia yake ni ya kama mapepe flani kwani huko nyuma liwahi kupata ujauzito akiwa shuleni lakini hata wakati anakuja kwangu inasemekana alikuwa ametoa mimba.
Baada ya kuishi kwangu takribani miezi sita niliona kama ameenza kubadilika sana niliamua kufanya uchunguzi ndipo siku moja nikawafumania akiwa na mume wangu kwenye kitanda changu, roho iliniuma sana nikatamani nimpige nikashindwa nikajikuta ninalia tu. Mwanaume akaniomba sana msamaha kiukweli nashinda cha kufanya labda wewe msomaji unaweza kunisaidia kwa kuchangia maoni yako chini. Ungekuwa wewe ungelifanyaje?

PATA TIKETI ZA SEMINA YA M&U:
Kwa yeyote  anayehitaji TIKETI za SEMINA YA M&U ya KUNA MAISHA NJE YA MAUMIVU YA MAPENZI NA JENGA UJASIRI SIMAMA TENA.
Unalipia Sh.7000/= kupitia TIGO PESA Na.0657486745 au M-PESA Na. 0767207156 unatuma majina yako kamili  kisha unatumiwa  NAMBA YA SIRI YA TIKETI YAKO  ambayo utaitumia siku ya semina.
Semina inafanyika Kijitonyama, Dar. Jumamosi ijayo. KARIBU SANA.
      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.