Sunday, August 7, 2016

Published 8/07/2016 08:00:00 AM by with 0 comment

MDUDU KUPE-3


Ilipoishia…
“Sawa lakini kama mimi ndiye msaada wako mbona kama kuna vitu unanificha,” Gregory alizidi kumbana Glory kwa maswali magumu.

Endelea …
“Hutaki kuniweka wazi kwani kila siku nakuona unazidi kukonda na kupauka sana mwili wako, yaani inaonekana kama una msongo mkubwa wa mawazo ambao unakusonga, tafadhali mpenzi wangu niambie mimi ndiye ninayekupenda, ninayekuheshimu, kukuthamini na kukulinda pia.

“Naomba uniambie na usinifiche kitu, kama kweli unapenda tuendelee kuwa wapenzi basi naomba unisaidie na mimi kuondokana na hili dukuduku nililonalo dhidi yako. Wewe siyo Glory yule niliyemzoea siku zote, umebadilika kwani hata uwezo wako wa kufikiri umekuwa mdogo sana,” alizidi kuongea Gregory.

“Hamna kitu mpenzi wangu, naomba uniamini, kama ningekuwa na kitu ningekwambia, mbona siku nyingine huwa nakwambia,” Glory alijifaragua lakini moyoni mwake akiwa anajishtukia.

Gregory akautoa kwa haraka mkono wake kwenye mkono wa Glory na kuamua kuondoka pekee yake huku akimuacha Glory.

Glory alijitahidi kumuita sana mpenzi wake lakini haikusaidia kitu wala hakugeuka nyuma zaidi ya kuendelea kusonga.

Gregory akakata kona akawa amepotea machoni mwa Glory. Ingawa Glory alijitahidi kumkimbilia lakini hakumuona, alichofanya ni kurudi mpaka nyumbani kwao na kuingia chumbani kwake, akafunga mlango na kuanza kulia kilio cha kimya kimya, akijilaumu kwa kile alichokifanya katika maisha yake.

Akawa anawaza amueleze ukweli mpenzi wake kilichokuwa kinamliza pale makaburini? Na kama akikijua atamsamehe na kuendelea na uhusiano wao kama zamani au ndiyo atakuwa ameuvunja uhusiano wake kwa mikono yake mwenyewe. Aliendelea kulia huku akigongagonga kichwa kidogo kwenye ukuta, mara akae kitandani ajilaze mara make.


Kiukweli Glory ni kama kachanganyikiwa na hajui afanye nini katika kumweleza mpenzi wake na amuelewe.
Kama si kufariki kwa wazazi wake nini kingine kilichomfanya alie kule makaburini, na kosa lipi hilo alilokosa akawa anamuomba Mungu amsamehe?

Usikose kujua undani wa kilio cha Glory pale makaburini…
Yawezekana umeteswa, umenyanyasika, umetelekezwa, umelizwa na umeachwa kisa kikiwa ni MAPENZI basi TUMAINI JIPYA laja usikose kuhudhuria Semina ya Mimi na Uhusiano (M&U). Siku ya Jumamosi, tarehe 27-8-2016.KIINGILIO:7000/= NA BITES.
MADA KUU:KUNA MAISHA NJE YA MAUMIVU YA UHUSIANO (XXLOVE)
JENGA UJASIRI SIMAMA TENA (UJASIRIAMALI).

Kwa maelezo zaidi au kupata tiketi yako mapema wasiliana nasi kwa namba 0657486745 au 0767207156.


      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.