Habari kaka G! Mimi ni mwanamke ninaishi Mtwara nina tatizo
ambalo linaniumiza sana kichwa, nilikua na mwanaume ambae tulikutana nikiwa
kidato cha nne ilikuwa mwaka 2008 tulipendana sana.
Mwaka 2012 akanipeleka kwako kwa ajili ya kunitambulisha lakini
baba yake hakunikubali kwa madai kabila langu ni tofauti na la kwao pia hafahamu
vizuri historia ya maisha yangu wala wazazi wangu.
Tulijaribu kumshawisha sana baba yake ila ilishindikana kilichofanyika walimtafutia
mwanamke wa kabila lake na kumuozesha na huo ndiyo ukawa mwisho wa mapenzi yetu
ingawa bado alikua ananipenda sana kwani alipopata upenyo ananipigia simu na tunaongea.
Alifanikiwa kupata mtoto mmoja kwenye ndoa yake lakini cha
ajabu mwaka huu wazazi wake wamenipigia simu na kuniambia wako tayari mtoto wao
anioe ila inabidi niende kwa mganga wa kienyeji wakanifungue, sijajua nikafunguliwe
nini?
Kwani mimi sina imani na mambo ya kishirikina ingawa jamaa
nampenda sana mpenzi wangu japo hana msimamo ila pia naogopa sana kujiingza
kwenye ushirikina sijajua niwakubalie au niwakatalie? Na ningoje Mungu anipe mume bora ambae hana
masharti kama hayo.
Tafadhali naomba ushauri wako kwa kukomenti chini ya mada
hii.
PATA TIKETI YA SEMINA YA M&U:
Habari, Kwa wale wanaohitaji TIKETI za SEMINA YA M&U
ya KUNA MAISHA NJE YA MAUMIVU YA MAPENZI NA JENGA UJASIRI SIMAMA TENA.
Unalipia Sh.7000/= kupitia TIGO PESA Na.0657486745 au
M-PESA Na. 0767207156 unatuma majina yako kamili kisha unatumiwa NAMBA YA SIRI YA TIKETI YAKO ambayo utaitumia siku ya semina.
Semina inafanyika Kijitonyama, Dar. Jumamosi ijayo.
(Admini Mimi na Uhusiano) KARIBU SANA.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.