Monday, August 8, 2016

Published 8/08/2016 08:00:00 AM by with 0 comment

MDUDU KUPE-2


Ilipoishia…
Kilio kikubwa cha Glory ni kutaka Mwenyezi Mungu amsamehe kwa yale aliyoyatenda katika uso huu wa dunia akiwa binti mdogo.

Kuna wakati hata yeye mwenyewe alikuwa anajiogopa kutokana na mambo ambayo amekwisha yafanya kwa umri huo alionao.


SONGA NAYO….

Gregory alivyojitahidi kuangalia vizuri alimuona Glory akiwa kasimama pembeni kukiwa na makaburi mawili roho ya huruma ikamuingia kijana huyo na kuanza kuhuzunika peke yake huku akili yake ikihamia ulimwengu mwingine kabisa, kumbe Glory huwa anakuja makaburini kwa ajili ya kuwaombea wazazi wake.

“Dah! Pole sana Glory,” Gregory alinyoosha mkono wake wa kulia kuelekea kwenye bega la Glory huku mkono wake wa kushoto ukishika kiunoni mwa Glory.
“Haaaa!” Glory akapiga mayowe kwani hakujua kama mpenzi wake Gregory alikuwa amemfuata mpaka makaburini.

“Gregory umeniogopesha, kwa nini usingenisubiri tu nyumbani” alisema Glory.
Wakati huo Gregory akiwa anacheka sana kwa namna ambavyo Glory alivyoogopa. “Haya pole sana Glory,” Gregory alimwambia Glory na kuzidi kumkumbatia kwa mikono yake miwili huku uso wake uliojaa upole akimwangalia Glory kwa huzuni nyingi na kumwambia.
“Pole sana mpenzi wangu Glory, sikujua kama huwa unakuja makaburini kwa ajili ya kusali, nimekuwa nikikufuatilia siku nyingi kila siku jioni jua likianza kuzama,” Gregory alimwambia Glory huku akipeleka uso wake kwenye midomo yake.
“Wewe Gregory unataka kufanya nini, hujui kama hapa ni makaburini, asante Gregory kwa faraja yako, yote ni mipango ya Mungu, nashukuru kwa kila jambo,’’ Glory alimjibu Gregory.
 Wakaanza safari ya kurudi nyumbani huku wakipiga stori za hapa na pale.


Pamoja na umri wa Glory kuwa ni mdogo sambamba na mwili wake, lakini maongezi yake yanaonyesha ni msichana mwenye busara na hekima kubwa.
Gregory alitamani kujua kuhusu maneno ambayo aliyasema Glory hapo awali kuwa: “Najua nimekukosea kwa kwenda kinyume na mapenzi yako lakini siyo mimi ni kwa sababu tu ya umaskini wetu.”


Gregory alimuuliza Glory: “Ulikuwa unamaanisha nini mpenzi wangu.” Swali hilo lilimfanya Glory ashtuke kwani hakutegema kama Gregory alisikia kilio cha maneno yake aliyokuwa analilia na kutubu pale kaburini.

“Hamna kitu, nilikuwa nalia tu kutokana na kuwakumbuka wazazi wangu, bado ninawakumbuka na kuwapenda ukizingatia msiba wenyewe ndiyo umetimiza mwaka mmoja na nusu tu na wameniachia mtihani mkubwa sana kwenye maisha yangu, na wewe pekee ndiyo msaada wangu,” alijibu Glory.

“Sawa lakini kama mimi ndiye msaada wako mbona kama kuna vitu unanificha,” Gregory alizidi kumbana Glory kwa maswali magumu.

Je, ni kitu gani hicho ambacho Gregory anahisi anafichwa na msichana anayempenda na kumwamini maishani mwake? Je, Glory alimuweka wazi mpenzi wake baada ya kubembelezwa? 
Usikose kesho.
Yawezekana umeteswa, umenyanyasika, umetelekezwa, umelizwa na umeachwa kisa kikiwa ni MAPENZI basi TUMAINI JIPYA laja usikose kuhudhuria Semina ya Mimi na Uhusiano (M&U). Siku ya Jumamosi, tarehe 27-8-2016.KIINGILIO:7000/= NA BITES.
MADA KUU:KUNA MAISHA NJE YA MAUMIVU YA UHUSIANO (XXLOVE)
JENGA UJASIRI SIMAMA TENA (UJASIRIAMALI).
Kwa maelezo zaidi au kupata tiketi yako mapema wasiliana nasi kwa namba 0657486745 au 0767207156.

      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.