SIMULIZI hii ina ukweli ndani yake na imemtokea mmoja wa wanaM&U na dhamira yake ya kuitoa simulizi hii ni kutaka watu wengine wajifunze kwa kile ambacho yeye amewahi kukutana nacho.
Bila shaka yawezekana hata wewe kuna mambo makubwa ambayo umewahi kuyafanya au kukutana naye unaweza kutushirikisha kwa siri kwa kutuma njia ya inbox au hata hadharani.
NB: Kwa mkasa, simulizi au ushauri wowote ule unabaki kuwa ni siri ya mhusika na M&U na kama tutaweka hadharani kwa ajili ya kujifunza, basi jina halisi la muhusika halitatajwa bila ridhaa yake.
Bila shaka yawezekana hata wewe kuna mambo makubwa ambayo umewahi kuyafanya au kukutana naye unaweza kutushirikisha kwa siri kwa kutuma njia ya inbox au hata hadharani.
NB: Kwa mkasa, simulizi au ushauri wowote ule unabaki kuwa ni siri ya mhusika na M&U na kama tutaweka hadharani kwa ajili ya kujifunza, basi jina halisi la muhusika halitatajwa bila ridhaa yake.
TWENDE PAMOJA…
Msichana Glory alionekana akiwa amenyoosha mikono yake miwili mbele kama vile mtu anayetaka kumpokea mtoto mchanga kutoka kwa mtu mwingine, lakini kwake haikuwa hivyo bali alikuwa akimlilia Muumba wake kwa uchungu wa hali ya juu huku machozi pamoja na kamasi laini vikimchuruzika kuelekea usawa wa pembeni mwa midomo yake laini.
Ukisikiliza kwa makini kilio cha msichana huyu ni cha kwikwi na simanzi kubwa sana.
“Ewe Mwenyezi Mungu, wewe ndiye unayejua maisha yangu nitakayoishi mimi na wadogo zangu, mara baada ya wazazi wangu kuiaga dunia na kuniachia wadogo zangu, umenitenga nao nikiwa bado ni binti mdogo ambaye nilikuwa nahitaji uangalizi wao.
“Naomba unisamehe, najua nimekukosea kwa kwenda kinyume na mapenzi yako lakini siyo mimi, bali ni kwa sababu tu ya umaskini wetu, maisha yaliniendea kombo wakati huo wadogo zangu wanahitaji pesa kwa ajili ya shule, wanahitaji kula, kuvaa na kadhalika, mimi sina pesa ndugu nao siuoni msaada wao.” Anaanza kulia tena msichana huyo mdomo mwenye miaka 19.
Kilio kikubwa cha Glory ni kutaka Mwenyezi Mungu amsamehe kwa yale aliyoyatenda katika uso huu wa dunia akiwa binti mdogo.
Kuna wakati hata yeye mwenyewe alikuwa anajiogopa kutokana na mambo ambayo amekwisha yafanya kwa umri huo alionao.
Mpenzi msomaji usikose kufuatilia wiki ijayo mkasa huu wa kweli na wakusikisha juu ya kile kilichoendela pale makaburini wakati Glory akilia.
Itaendelea … KESHO
Yawezekana umeteswa, umenyanyasika, umetelekezwa, umelizwa na
umeachwa kisa kikiwa ni MAPENZI basi TUMAINI JIPYA laja usikose kuhudhuria
Semina ya Mimi na Uhusiano (M&U). Siku ya Jumamosi, tarehe
27-8-2016.KIINGILIO:7000/= NA BITES.
MADA KUU:KUNA MAISHA NJE YA MAUMIVU YA UHUSIANO (XXLOVE)
JENGA UJASIRI SIMAMA TENA (UJASIRIAMALI).
JENGA UJASIRI SIMAMA TENA (UJASIRIAMALI).
Kwa maelezo zaidi au kupata tiketi yako mapema wasiliana nasi
kwa namba 0657486745 au 0767207156.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.