SEHEMU YA 11
“Kuwa huru tu
kaka, hapa nyumbani tumebaki wawili tu mimi na dada,” Doreen alimwambia Nelly
huku akiwa anakwenda sehemu ya kulia chakula palipokuwa na kabati kubwa la vioo
lililokuwa na vyombo.
Endelea…
Kwa kuwa muda huo, msichana huyo alivaa pensi
iliyombana vyema na kusababisha wowowo lake la kiuchokozi kuonekana na bla
nyepesi mfano wa singilendi iliyoonesha viembe sindano vyake, Nelly
akachanganyikiwa kabisa.
“Aaa…duuu…aaa…,” Nelly alijikuta akiguna akiwa
amelitumbulia macho eneo la nyuma la Doreen na kushindwa kuendelea kunywa
juisi.
Doreen ambaye hakuwa na habari na kilichokuwa kikijiri
nyuma yake, alipolifikia kabati la vyombo alisukuma vioo vya kusilaidi na kutoa
glasi lakini ile anageuka Nelly alijifanya anakunywa juisi.
“Ngoja na mimi nikusaidie,” Doreen alimwambia Nelly
wakati akimimina juisi juisi kwenye glasi yake kisha akaketi kwenye sofa
aliloketi Nelly.
Kitendo cha msichana huyo kuketi karibu na sharobaro
Nelly, kijana huyo alizidi kuchanganyikiwa ndipo Doreen alimwuliza kama kweli
alikuwa fundi au alikuja pale kumpeleleza baba yake.
“Hapana sista, mimi nije kumpeleleza baba yako ili
iweje wakati simfahamu na ndiyo mara yangu ya kwanza kufika hapa,” Nelly
alimwambia Doreen.
“Ulivyo na kazi unayoifanya vitu viwili tofauti lazima
nikutulie shaka,” Doreen alimwambia Nelly.
“Naomba usinifikirie hivyo, mimi siyo mpelelezi,”
Nelly alimwambia Doreen.
Baada ya Nelly kumhakikishia hivyo Doreen, msichana
huyo alitabasamu na kumwambia kama ni kweli itakuwa vizuri ndipo alimwuliza
sababu za kuchagua kazi ya ufundi.
“Maisha tu dada, ila nilitamani sana kukaa ofisini
niwe nafanya kazi kwa kutumia kompyuta lakini ndiyo hivyo,” Nelly alimwambia
Doreen.
Kufuatia kijana huyo kumwambia hivyo Doreen, msichana
huyo alimwuliza alifika kidato cha ngapi, Nelly alimwambia cha nne na kumweleza
kila kitu hadi kufikia hatua ya kuwa pale.
“Unataka kuniambia leo ndiyo kwa mara yako ya kwanza
kufanya kazi ya ufundi?” Doreen ambaye alimuonea huruma Nelly alimwuliza.
“Ndiyo hivyo,” Nelly alimjibu.
Baada ya kijana huyo kujibu hivyo, Doreen alikubaliana
naye kwani alimuona jinsi alivyokuwa akijinyoosha kila alipochota mchanga na
kuutupia eneo aliloelekezwa na Zakayo.
“Oke, sasa sina shaka na wewe, naomba nikuongeze
juisi,” Doreen ambaye alipania kufikia hatua f’lani na Nelly alimwambia.
“Nashukuru sista inatosha,” Nelly alimwambia Doreen.
Licha ya kukataa, Doreen alimimina juisi na kujaza
glasi aliyokuwa akitumia Nelly, lengo lake lilikuwa kumchelewesha kwani
aliamini kitendo cha kuwa pamoja na Nelly angemtongoza tu!
“Ila wewe dada ni mkarimu sana, nashukuru kwa
kunijali,” Nelly alimwambia Doreen.
Usikose kuhudhuria Semina ya Mimi na Uhusiano
(M&U). Mada Kuu: “KUNA MAISHA NJE YA MAUMIVU YA MAPENZI.” Itakayofanyika
Agosti, 27 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Malaika Hall, Kijitonyama. kwa maelezo
zaidi wasiliana nasi kwa namba 0657486745 au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na
Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.