Ilipoishia…
Kiukweli Glory ni kama kachanganyikiwa na hajui afanye nini katika kumweleza mpenzi wake na amuelewe.
Kama si kufariki kwa wazazi wake nini kingine kilichomfanya alie kule makaburini, na kosa lipi hilo alilokosa akawa anamuomba Mungu amsamehe?
SONGA NAYO…
Glory alijiuliza sana maswali kuhusu kumueleza ukweli Gregory wake lakini moyo wake ulikuwa ukijawa na shaka sana kwa kuonekana si mtu mwema kwenye uhusiano wake jambo lililomfanya ajione mkosaji asiye stahili hata kusamehewa na mtu yeyote yule mwenye kujua ukweli.
“Gregory naomba unisamehe mpenzi wangu najua nimekukosea sana, baada ya kifo cha wazazi wangu wewe ndiye uliyekuwa msaada mkubwa sana kwangu, wewe ndiye uliyejitolea kuilisha familia yangu, nakupenda sana John ila naomba msamaha wako mpenzi wangu.
“Sina namna Gregory kama unazidi kung’ang’ania kuujua ukweli itabidi nikwambie tu,” Glory alijikuta akiwa anawaza kiasi cha kupitiwa na usingizi mzito.
Wadogo zake baada ya kutoka kanisani kwenye mafundisho ya kipaimara walifika nyumbani wamechelewa wakati huo kigiza kilikua kimeshaanza kuingia, walimtafuta sana dada yao lakini hawakumuona, ndipo wakapata wazo la kwenda kusukuma mlango wa dada yao kuona kama atakuwa yumo ndani, lakini wakashangaa kukuta mlango umefungwa na walipochunguza kwa makini wakabaini umefungwa kwa ndani, hivyo wakaanza kuugonga huku wakiita jina la dada yao.
“Dada Glory! Dada! Waliita kwa muda wakiwa wamekata tamaa ya kuita, ndipo wakashanga mlango unafunguliwa na dada yao akiwa anaonekana ametoka kwenye lepe zito la usingizi.
“Poleni sana wadogo zangu, kichwa kinaniuma sana niliingia ndani kupumzika ndiyo nikapitiwa na usingizi,” alisema Glory.
Glory alijua watakuwa wamegonga sana mlango na alipenda kuwapa kauli zenye matumaini kuliko kuwakalipia kwani aliamini kufanya hivyo ni sawa na kuwakumbusha kipindi walichokuwa wanaishi na wazazi wao wakati hawajaaga dunia kwani waliwapenda na kuwajali sana.
Itaendelea kesho…
Yawezekana umeteswa, umenyanyasika, umetelekezwa, umelizwa na
umeachwa kisa kikiwa ni MAPENZI basi TUMAINI JIPYA laja usikose kuhudhuria
Semina ya Mimi na Uhusiano (M&U). Siku ya Jumamosi, tarehe
27-8-2016.KIINGILIO:7000/= NA BITES.
MADA KUU:KUNA MAISHA NJE YA MAUMIVU YA UHUSIANO (XXLOVE)
JENGA UJASIRI SIMAMA TENA (UJASIRIAMALI).
JENGA UJASIRI SIMAMA TENA (UJASIRIAMALI).
Kwa maelezo zaidi au kupata tiketi yako mapema wasiliana nasi
kwa namba 0657486745 au 0767207156.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.