Wednesday, August 17, 2016

Published 8/17/2016 08:43:00 AM by with 0 comment

NELLY MUOSHA MAGARI WA POSTA SEHEMU YA 10


Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale mtoto mkali Doreen alipombembeleza Nelly kwa sauti nyonyoro kwamba aliogopa nini kuingia ndani na kumsihi aingie kwani hakukuwa na tatizo. Je, baada kijana huyo sharobaro kuambiwa hivyo alisemaje? Tuwe pamoja kwenye utamu huu…
Endeleea..
Kutokana na sauti nyororo ya kuhamasisha aliyoitoa Doreen, Nelly alijikuta akiwa jikoni mwa akina Doreen ambapo msichana huyo alimuongoza mpaka sebuleni kwao, kutokana na nguo aliyovaa kuchafuka kwa mchanga akawa hajui aketi wapi.
“Karibu ukae kwenye kiti,” Doreen alimwambia Nelly.
“Hapana sista wewe nipe nitakunywa wima, si unaona nilivyochafuka!” Nelly alimwambia Doreen.
Licha ya Nelly kutoa jibu hilo, Doreen ambaye ghafla alitokea kuvutiwa na kijana huyo kimapenzi kutokana na kupita muda mrefu bila kuduu alimlazimisha Nelly kukaa na kusisitiza kwamba hata sofa zingechafuka angemwambia Anne azifute.
Kitendo cha kubembelezwa kukaa na mtoto huyo ‘mtamu,’ Nelly alikaa sofani kitendo kilichomfurahisha sana Doreen ambaye alikwenda sehemu ya kulia chakula palipokuwa na jokofu na kuchukua jagi pamoja na glasi.
Alipofika alipoketi Nelly alizogeza stuli iliyokuwa pembeni ya kochi na kuiweka glasi, akafungua jagi na kumimina juisi nzito ya embe, akachukua glasi na kumkabidhi Nelly aliyebakia kaduwaa.
“Wewe si ulitaka maji, mimi nimependa unywe hii juisi,” Doreen mtoto aliyeumbwa haswa na kujaliwa kuwa na makalio f’lani hivi ya kiuchozi alimwambia Nelly.
“Da! Sikutegemea kama leo nitakutana na sapraizi ya namna hii,  sina cha kuongezea zaidi ya kushukuru kwa ukarimu huu ambao sijapata kuuona,” Nelly alimwambia Doreen.
Wakati Nelly na Doreen wakipiga stori ndani, si fundi Yassin, Zakayo wala Haruni aliyekumbuka habari za Nelly kwani wakati huo walikuwa bize kwa kazi ya kuweka malumalu.

“Kuwa huru tu kaka, hapa nyumbani tumebaki wawili tu mimi na dada,” Doreen alimwambia Nelly huku akiwa anakwenda sehemu ya kulia chakula palipokuwa na kabati kubwa la vioo lililokuwa na vyombo.

Usikose kuhudhuria Semina ya Mimi na Uhusiano (M&U). Mada Kuu: “KUNA MAISHA NJE YA MAUMIVU YA MAPENZI.” Itakayofanyika Agosti, 27 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Malaika Hall, Kijitonyama. kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba 0657486745 au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
 Usikose kesho muda kama huu…
      edit

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.