Anko G. samahani mimi nina jambo linanitesa sana mim ni mdada mkazi wa Kagera linalonisibu nilikuwa na mpenzi mwanzoni mwa mwezi wa nne baada ya kuingia kwenye mahusiano na kuwa naye karibu nimegundua hana ustaarabu hata kidogo, ana tabia chafu sana nikaamua kumuweka wazi kwamba kama hata badilika siwezi kuwa naye lakin hakubadilika nikaamua kumuacha.
Nimekaa muda baadaye nikampata kaka mwingine aliniambia hana mke, nikaanza naye uhusiano, yule kaka wa zamani niliyemuacha amèfanya uchunguzi akagundua kuwa natembea na mwanaume mwingine alichofanya kwa kuwa anamjua huyo mkaka akamtafuta mke wake akamwambia kuwa natembea na mume wake.
Alichofanya akampa yule mwanamke na namba yangu ya simu na huyo mdada ananitafuta, maana juzi amenipigia simu kwamba tuonane , Je, nifanye nini na mimi sikuwa najua kama ni mume wa mtu?
Kwa habai, ushauri, simulizi, chombezo, mada za mahaba na mikasa ya kweli ya mapenzi jiunge na M&U WhatsApp kwa namba 0657486745. kwa mada za kila siku. au tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com
Nimeteswa, nimelizwa,
nimenyanyasika, nimeumizwa kisa kikiwa ni mapenzi ila kwa Semina ya Mimi na
Uhusiano (M&U) YA KUNA MAISHA NJE YA MAUMIVU YA UHUSIANO (XXLOVE).
JENGA UJASIRI SIMAMA TENA (UJASIRIAMALI). Siku ya Jumamosi, tarehe 27-8-2016.
SIYAKUKOSA KWA KIINGILIO:7000/= NA BITES.
Kwa maelezo zaidi au kupata
tiketi yako mapema wasiliana nasi kwa namba 0657486745 au 0767207156.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.