Wednesday, May 31, 2017

Published 5/31/2017 04:28:00 PM by

MUNGU NDIO UPANGA MUDA WA KUPATA MTOTO

Katika kuzungumzia manyanyaso, matusi na mambo mengi ya ajabu ambayo wanakutananayo wanandoa, hususan wanawake ambao wamekuwa wakibebeshwa mzigo mkubwa na mzito na wanaume wao.
Kinachonishangaza ni kuona binadamu anajivisha mamlaka ya kumtaka mwenza wake awe na mtoto ilihali anajua kabisa kuwa hilo hana mamlaka nalo isipokuwa Mwenyezi Mungu. Si ajabu pengine anayelalamika na kutukana kuwa anahitaji mtoto, yeye mwenyewe hana uhakika kama ni mzima kwa upande wa viungo vya uzazi au mwingine naye unakuta hata yeye hajajua kama akiolewa atapata mtoto au lah!
Mara nyingi chanzo cha tatizo hilo, lawama nyingi hubebeshwa upande mmoja wa wanawake, kwa kuamini kuwa mwanaume yeye huwa siku zote yuko sawa, hawezi kuwa na upungufu katika kukamilisha utungaji wa mimba.
Mbaya zaidi mwanaume anapojiona kuwa faragha yuko vizuri, ndiyo basi kabisa anaona hana sababu ya kushindwa kumlaumu mwanamke kuwa ndiye mwenye matatizo ya kutokushika mimba.


Moja kwa moja anaanza
 kulalamika na kumtuhumu mwenza wake kuwa yawezekana alitoa mimba nyingi kipindi cha usichana wake, mgumba au alitembea na mume wa mtu akafanyiwa figisufigisu.
Kumlaumu mwanamke kuwa ni chanzo cha mwanaume kukosa mtoto ni kumuonea. Kumlaumu mwenza wako kuwa ameshindwa kukuzalia mtoto bila wewe kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu ni unyanyasaji wa kijinsia na ni kuingilia uumbaji wa Mungu. Hata kama akionekana ana tatizo, si vyema kumnyanyasa.
Zipo changamoto zinazowakumba wanandoa kwenye ndoa zao ikiwemo ugomvi wa mara kwa mara, malumbano ya hapa na pale na usaliti. Baadhi ya wanaume wamechukulia tatizo la kukosa mtoto kwa wenza wao kama fimbo ya kuwachapia wenza wao. Kila anapokosea jambo f’lani basi anaanza kusimangwa hata kama mwenye kosa ni mwanaume, lakini kibao kinamgeukia mwanamke.
Suala la mwanamke kutoshika mimba, pamoja na kwamba hata mwanaume anaweza akawa hana uwezo wa kuzalisha mbegu zenye uwezo wa kutengeneza mtoto, ni changamoto kwenye ndoa nyingi katika jamii.
Sehemu kubwa ya jamii inaamini kuwa wanandoa ambao wametimiza mwaka mmoja kwenye ndoa yao basi wanapaswa wawe na mtoto. Kama si mtoto, basi angalau mwanamke awe na mimba changa au kitumbo kiwe kimeanza kuonekana.
Ndugu yangu, si lazima kila ndoa iliyotimiza mwaka mmoja iwe na mtoto au mwanamke awe mjamzito. Suala la kupata mtoto ni uamuzi au majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Wewe kama mwanamke huna mamlaka nalo. Wewe kama mwanaume, umebahatika kufunga ndoa na kuishi na mwenza wako, basi shukuru Mungu na hata suala la mtoto siku zote ni majaliwa ya Mungu na si upendavyo wewe.
Nayahisi maumivu makali anayopata mwanamke ambaye hana mtoto na mumewe badala ya kumfariji anageuka kuwa adui yake. Anageuka mtu wa kumnyanyasa. Inauma, inasikitisha na inatesa sana mioyo ya wanawake wengi.


Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

CHANZO: GPL
Read More
      edit

Saturday, May 27, 2017

Published 5/27/2017 12:13:00 PM by

WOLPER AZUNGUMZIA KUKOMOREWA KIMAPENZI

Malkia wa filamu, Jacqueline Wolper amefunguka kueleza moja na sababu ya mahusiano yake na wanaume wengi kushindwa kudumu kwa muda mrefu.


Muigizaji huyo ambaye ameachana na msanii Harmonize miezi kadhaa iliyopita, amedai kuna baadhi ya wasichana wanaingilia mapenzi yake ili kumkomoa.
“Mimi ni kama nina kipaji cha kukomeshwa kwenye mapenzi kwa sababu kipaji ninachokivumbua mimi wenzangu wanataka wapite hapo hapo ili kunikomoa. Ni kwamba nina kipaji cha kukomeshwa lakini huyo anayenikoa unakuta hajui mimi nimepambana vipi kumtengeneza mtu anipendae” alisema Wolper.

Licha ya Wolper na Harmonize kutoweka wazi sababu ya kuachana, lakini stori ambazo ziko mtaani zinadai Harmonize amemuacha muigizaji huyo baada ya kupata mwanamke wakizungu.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.


Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa

Read More
      edit
Published 5/27/2017 11:54:00 AM by

MAGAZETI YA LEO MAY 27, 2017











Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.


Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Read More
      edit

Friday, May 26, 2017

Published 5/26/2017 10:47:00 AM by

MAGAZETI YA LEO MAY 26, 2017







Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.


Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Read More
      edit

Thursday, May 25, 2017

Published 5/25/2017 05:46:00 PM by

NJIA ZA UHAKIKA YA KUWA NA KESHO YENYE MAFANIKIO

Makosa tuliyofanya tukashindwa kufaulu masomo, au tukafukuzwa kazi, au biashara zetu zikafa. Wakati uliopita umebeba mengi na ndiyo umekufikisha hapo ulipo sasa. Maamuzi uliyofanya siku zilizopita huko nyuma, ndiyo yamekufikisha hapo ulipo. Watu uliokuwa karibu nao siku zilizopita, ndiyo wamekusaidia kujenga maisha uliyonayo sasa. Mawazo uliyoruhusu yatawale akili yako siku za nyuma, ndiyo yamekaribisha kila ulichonacho sasa kwenye maisha yako. Kwa kifupi upo hapo ulipo sasa, kwa sababu ulichagua hivyo siku zilizopita. Najua utabisha kama bado unaamini wazazi wako ndiyo wamekufikisha hapo, au serikali ndiyo imekufikisha hapo, ila usikate tamaa, nitakuonesha namna ya kutoka hapo ulipo sasa muda siyo mrefu.

Mbili; wakati uliopo sasa.

Wakati mwingine ambao unao kwenye maisha yako, ni wakati uliopo sasa, wakati huu, hivi unavyosoma hapa sasa, ndiyo wakati ambao unao. Huu ni wakati muhimu sana kwa sababu ndiyo unatengeneza kesho yako. Kama tulivyoona kwenye wakati uliopita, ndiyo umetengeneza wakati uliopo sasa, wakati ulionao sasa ndiyo unatengeneza wakati ujao. Kila unachofanya sasa, hapo ulipo unatengeneza matokeo ya kesho. Namna unavyofanya kazi au biashara yako, ndiyo mbegu unayoipanda kwa ajili ya kesho. Mawazo unayoruhusu yatawale akili yako sasa, ndiyo yanatengeneza kesho yako. Na hata watu wanaokuzunguka sasa, ndiyo wanakusaidia kuijenga kesho yako. Chochote unachofanya sasa, hakitaenda bure, bali kitaijenga kesho yako, iwe ni kitu kizuri au kibaya.

Tatu; wakati ujao.

Huu ni wakati ambao bado hatujaufikia, ni wakati ambao unakuja, na hatuna uhakika utakuwaje wakati huo. Hakuna mtu yeyote amewahi kufanikiwa kutabiri kwa uhakika wa asilimia 100 kwamba wakati unaokuja utakuwaje. Hakuna ambaye amewahi kuiona kesho, lakini tuna matumaini itakuwa bora, na mambo yatakuwa kama sasa au bora zaidi. Wakati ujao ni matumaini kwetu, ndiyo unaotusukuma tuweke juhudi zaidi leo, ili wakati huo uwe bora sana. Ndiyo maana tunakazana kuwekeza, kuweka akiba na mengine ili kuhakikisha kesho, kwa vyovyote itakavyokuja, basi tutaendelea kuwa vizuri. Kesho inatusukuma kuchukua hatua leo, ili inapokuja, tusiwe kwenye wakati mgumu. 



Tatizo kubwa tunaanza kulitengeneza hivi.

Sasa lipo tatizo kubwa sana kwenye hizi nyakati tatu, tumekuwa hatuziishi kama ambavyo tumezielezea hapo juu, kwamba nyakati zilizopita ni jana, wakati uliopo ni leo na wakati ujao ni kesho. Badala yake tumekuwa tunavuruga kila wakati na mbaya zaidi kujinyima wakati wa kuishi ni sasa.

Picha huwa linaanza pale tunapofikiria wakati uliopita, makosa ambayo tumefanya, fursa ambazo tumezikosa, na kujiona kama tumepoteza sana. Tunajilaumu kwa nini tulifanya au hatukufanya kitu fulani. Tunajitesa kwa makosa tuliyoyafanya huko nyuma. Na yote haya, tunayafanya kwenye wakati tulionao sasa, ambao tulipaswa kufanya mambo ya sasa.

Hatuishii hapo, bali tunaiangalia na kesho pia, wakati ujao. Tunaangalia wakati huo kwa hofu kubwa, tukiona mambo yatazidi kuwa mabaya, hali itazidi kuharibika, maisha yatazidi kuwa magumu na hatutaweza tena kupiga hatua. Tunajenga picha moja mbaya na ya hatari sana, picha inayotufanya tushindwe kabisa kupiga hatua yoyote ile, na kubaki kama tumepingwa sindano ya ganzi. Hili linachangia zaidi kuharibu wakati tuliopo sasa.

Kwa kuchanganya yale tuliyofanya au kutokufanya wakati uliopita, na kufikiria mabaya zaidi kwa wakati ujao, tunajikuta hata wakati tulionao sasa hatufanyi chochote. Hatuchukui hatua yoyote ambayo ingeweza kubadili hali ya mambo hapo kesho, badala yake tunajaza akili yetu mawazo ambayo hayawezi kutusaidia. Mawazo ambayo yanatupa hofu zaidi ya kufanya, na tunabaki hatujui tufanye nini. Hapa ndipo wengi hukata tamaa na hata wengine kufikia kukatisha uhai wao.

Ipo njia ya kuhakikisha kesho yako inakuwa na mafanikio makubwa.

Na njia hiyo siyo ngumu kama unavyofikiri, bali ni rahisi sana, na ni kuchagua kuishi leo.

Kwenye njia hii, unachagua kuishi leo, kwa sababu kile unachofanya leo ndiyo kinaandaa kesho yako. Kwa njia hii unatambua yale yaliyopita, lakini unakubali kwamba haijalishi utafanya nini, huwezi kubadili chochote ambacho kimepita, huwezi kurudi na kufuta makosa yaliyopelekea kufeli, kufukuzwa kazi au biashara kufa. Huwezi kurudi nyuma na kuzichukua zile fursa ambazo zilikupita. Lakini unajua kwamba kwa kufanya kitu leo, kwa kuchukua hatua leo, basi unaitengeneza kesho yako vizuri zaidi. Unachofanya kwa wakati uliopita ni kujifunza na kusonga mbele.



Pia kwa wakati ujao, ambao tumekuwa tunautengenezea hofu, tunakubali kwamba hatuwezi kuujua kwa uhakika, na hatuwezi kuuishi kabla haujafika. Hivyo kupoteza muda mwingi kuufikiria kwa hofu, hakutatusaidia lolote kwa sasa. Hivyo tunautumia kama hamasa ya sisi kufanya kitu leo.

Kazi kubwa kwetu ni kuishi kwenye wakati tuliopo sasa, kuchukua hatua kwenye wakati huu, kufanya kitu sasa. Kuyaangalia kwa kina mawazo ambayo tumeruhusu yatawale akili yetu sasa, je ni mawazo yanayotujenga au kutubomoa? Ni mawazo chanya au hasi? Pia tuangalie wale ambao wanatuzunguka, je kuna mahali popote wanaenda na maisha yao au wapo wapo tu. Ni watu ambao wana msaada kwetu au wanaturudisha nyuma? Ni muhimu pia kuangalia kila jambo unalofanya sasa, kila hatua unayopiga sasa na kuona kama ina mchango wowote kwenye kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi leo na siku zijazo.

Namna unavyofanya kazi yako na hata biashara yako, je inaongeza ufanisi zaidi?

Unatengeneza thamani zaidi?

Ili kuishi vizuri leo, na kuweza kuitengeneza kesho ambayo ni bora zaidi, basi zingatia yafuatayo;

1. Kuwa na maono makubwa ya siku zijazo, mwaka mmoja kutoka sasa, miaka mitano, miaka kumi na kuendelea. Siyo lazima uyafikie kama yalivyo, lakini yatakusukuma kuchukua hatua.

2. Hakikisha kuna hatua unachukua leo, ambayo itakufanya kuwa bora zaidi ya ulivyokuwa jana.

3. Usikubali kuzungukwa na watu ambao hawajui wapi wanakwenda, kaa mbali na watu hasi.

4. Usipoteze muda wako kujutia makosa uliyofanya huko nyuma, au fursa ambazo hukuzichukua.

5. Tumia muda wako wa leo vizuri, usipoteze hata dakika moja, poteza fedha utazipata nyingine, poteza muda na hautaupata tena.
Fanya haya rafiki, na kesho yako, kwa hakika haitakuwa kama ilivyo leo, au ilivyokuwa jana. Japo huwezi kujua kwa hakika itakuwaje, lakini itakuwa bora zaidi.


BY Tatu Kiondo
Read More
      edit
Published 5/25/2017 05:10:00 PM by

MAMBO YATAKAYOKUWEZESHA KUFIKIA UTAJIRI KUPITIA UJASIRIAMALI



Inawezekana lengo lako siyo kuwa bilionea, lakini kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho kuhusu wewe ni kwamba unahitaji utajiri. Unahitaji kuwa na uhuru wa kifedha ili uwe huru kwenye maamuzi yako ya kimaisha. Hivyo basi, kwenye makala ya leo nakwenda kukushirikisha mambo saba muhimu yatakayokuwezesha kufikia utajiri kupitia ujasiriamali.


Mambo hayo ni kama yafuatayo;

1. Jifunze kuwaamini watu.

Hutaweza kufikia utajiri kupitia ujasiriamali iwapo kila kitu utafanya mwenyewe. Vitu vingi unavyofanya unahitaji kuwapa wengine wakusaidie na wewe uweke nguvu zako kwenye yale ambayo ni muhimu zaidi. Sasa kama huwezi kuwaamini watu na kuona wanaweza kufanya kazi nzuri, hutaweza kuwapa majukumu yako na badala yake utang’ang’ania kufanya kila kitu peke yako na kuishia kushindwa.

Jifunze kuwaamini watu na wape majukumu ambayo wanaweza kukusaidia. Kufikia utajiri unahitaji msaada wa wengi, jua namna ya kufanya kazi vizuri na watu wengi.


2. Fanya vizuri sana kile ulichochagua kufanya.

Hakuna tajiri ambaye anafanya mambo kwa kubahatisha. Wote ambao wanafanikiwa sana kwenye ujasiriamali wanafanya vizuri sana kile ambacho wamechagua kufanya. Wanaweka juhudi kubwa kuongeza thamani na kutengeneza matokeo bora kabisa. Kwa njia hii watu wanawaamini na kuwategemea kupitia kile wanachofanya.

Jitengenezee jina kwa kufanya vizuri sana kile ambacho umechagua kufanya. Hakikisha kuna kitu kinakutofautisha wewe na wengine ambao wanafanya kama unachofanya wewe.

3. Toa zaidi ya unavyotegemea kupokea.

Badala ya kuuliza dunia inakupa nini, jiulize unaipa nini dunia. Haijalishi wateja wanakulipa kiasi gani, hakikisha unawapa vitu vyenye thamani kubwa, vitu ambavyo ni bora kabisa.

Hakikisha mteja akiangalia anachokulipa na unachompa, anaona kama amekuibia. Na wala siyo lazima uingie hasara kwenye kufanya hivyo, inaweza kuwa ni ile huduma ya kipekee kabisa anayoipata, ambayo hajawahi kuipata kwingine popote.
Ipe dunia zaidi ya unavyotegemea kupata, na dunia italazimika kukulipa wewe kwa kadiri ya unavyotoa.

4. Sahau majuto.

Utafanya makosa mengi sana kwenye safari yako ya ujasiriamali, ambayo yatakukwamisha kufanikiwa. Lakini kupoteza muda kufikiria makosa hayo ya nyuma, hakutakuwa na msaada wowote kwako. Kujutia yale uliyofanya na yakakurudisha nyuma, ni kupoteza muda wako.

Kwa makosa yoyote ambayo ulishafanya, jifunze na songa mbele. Una mengi sana ya kufanya ambayo yapo mbele yako, usipoteze muda kuangalia nyuma, badala yake kazana kusonga mbele.

5. Jifunze kukubali kupoteza.

Hakuna mtu anayeshinda kila wakati. Hata wajasiriamali unaowaona wana mafanikio makubwa, kuna wakati walishindwa, kuna wakati walipoteza. Kabla hujafanikiwa, utapitia vikwazo na changamoto nyingi. Lazima ukubali kupoteza na kujifunza ili kuweza kusonga mbele.

Pale unapoanguka usikae chini na kusema kwa nini mimi, badala yake kubali kilichotokea na simama kusonga mbele. Wale wasiokubali kupoteza hutafuta mtu wa kumlaumu kwa kilichotokea, wale wanaofanikiwa wanakubali, wanajifunza na kisha wanasonga mbele, wakifanya kwa ubora zaidi.

6. Chukua jukumu la maisha yako na mafanikio yako.

Hakuna ambaye atakuja kukutoa hapo ulipo kama wewe mwenyewe hutaamua kutoka hapo.

Na hata unaposhindwa, usikimbilie kutafuta nani kasababisha, hakuna mkono wa mtu yeyote ila wako, ambao unapelekea wewe kushindwa. Hivyo shika jukumu la maisha yako, pambana kufikia ndoto zako. Hakuna atakayekuletea utajiri mezani, na wala hakuna njia ya mkato ya kuufikia. Lazima ukubali kuweka kazi na muda wa kutosha ili kupata kile unachotaka.

7. Una vitu viwili tu, NENO lako na JINA lako.

Jifunze kuwa mwadilifu na mwaminifu, kila neno lako linabeba jina lako. Jifunze kutimiza kile ambacho unaahidi. Hakikisha matendo yako yanaendana na maneno yako. Unahitaji kujijengea uaminifu usiotiliwa shaka, ili watu waweze kukuamini na kufanya biashara na wewe na hata kukusaidia. Usijihusishe kwenye jambo lolote ambalo litaharibu sifa yako na jina lako. Usishiriki mpango wowote wa mkato wa kufikia mafanikio, mipango hii mingi siyo halali na itaishia kuharibu mafanikio yako.

Wapo ambao wanafanikiwa na kuwa matajiri kwa njia ambazo siyo halali, lakini hawawezi kujivunia utajiri huo mbele ya wengine. Kibaya zaidi utajiri wa aina hiyo umekuwa haudumu muda mrefu. Wewe huhitaji kupita njia hiyo, kwani unaweza kujijengea utajiri kwa njia za halali kabisa, ukianzia chini kabisa. Fanyia kazi mambo haya saba tuliyojifunza hapa na hakika maisha yako hayatabaki hapo yalipo sasa. Kama kuna ambavyo tayari unafanyia kazi, endelea kuboresha zaidi na vifanye kuwa misingi ya maisha yako.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.


Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa



 BY Tatu Kiondo
Read More
      edit
Published 5/25/2017 04:40:00 PM by

FAIDA ZA KUFANYA TENDO LA NDOA




Tendo la ndoa tangu uumbaji lililengwa kati ya mwanaume na mwanamke waliofunga ndoa, sasa hivi dunia imebadilika sana kiasi kwamba tendo hili sio lazima kuliita la ndoa tena. watu wengi wamekua wakishiriki tendo la ndoa bila kujua faida zake.lakini tendo la ndoa lina faida nyingi sana kiafya na kisaikolojia. hivyo kama wewe una mke, mchumba au mpenzi halafu kila siku unampa sababu za kutoshiriki basi huenda hujui faida zake. hebu tuzisome kama ifuatavyo..

Huondoa msongo wa mawazo; kipindi cha tendo la ndoa mwili hutoa hormone inayoitwa kitaalamu kama endophirn ambayo huleta furaha.kila aliyeshiriki tendo la ndoa atakua shahidi kama una msongo wa mawazo sana ukaenda kufanya tendo hili utajikuta unajisikia vizuri sana,

Hupunguza presha ya damu; wakati wa tendo la ndoa damu inapita kwa kasi sana kwenye mishipa ya damu na kuondoa vikwazo kama mafuta, lehemu na kunyoosha mishipa iliyosinyaa.utafiti unaonyesha tendo la ndo hushusha presha ya chini kitaalamu kama diastolic pressure.

Huongeza kinga ya mwili; askari wa mwili kwa jina immunoglubin hutolewa na mwili kupambana na magonjwa wakati wa tendo la ndoa, kama huamini basi shiriki tendo la ndoa ukiwa na mafua na baadae utashindwa kuelewa mafua yameenda wapi.

Huimarisha mahusiano; kuna homoni ya furaha na uzazi inaitwa oxytocin homoni, homoni hii hutengenezwa na mwili kipind cha tendo la ndoa.kama umekaa kwenye mahuasiano muda mrefu utagundua kwamba ikitokea umegombana na mpenzi wako halafu mkafanya tendo la ndoa basi ugomvi unaisha bila hata kuongelea swala lililowagombanisha.

Hupunguza uwezekano wa kupata kansa ya tezi dume; utafiti uliofanyika nchini australia uligundua kwamba wanaume wanaoshiriki tendo la ndoa angalaua mara 21 kwa mwezi wako kwenye hatari ndogo sana ya kupata kansa ya tezi dume kuliko wale wasioshiriki hivyo kama mpenzi au mke wako hakupi ushirikiano basi atakuletea kansa.

Husaidia kupata hedhi kwa wakati; tendo la ndoa huweka homone za uzazi kitaalamu kama oestrogen na progesterone kwenye kiwango sawa. hii husaidia kupata siku zako kwa wakati na bila maumivu.kimsingi tendo la ndoa husaidia sana kuliko vidonge vya uzazi ambavyo humezwa na watu ambao hawaoni siku zao.

Huleta usingizi wa kutosha; hii haihitaji ubishi au ushahidi mara nyingi baada ya kushiriki tendo la ndoa hata kama ni mchana kila mtu hupata uchovu fulani na kujikuta unapitiwa na usingizi kwa muda mrefu.

Sehemu ya mazoezi;tendo la ndoa lina faida zote ambazo mtu anayefanya mazoezi anazipata ikiwemo kupungua uzito, kua na afya bora hata kuondoa kitambi kwani wakati wa tendo la ndoa mapigo ya moyo huongezeka, kasi ya upumuaji hua juu na kua sawa na mtu wa mazoezi.

hukufanya uishi muda mrefu; moja ya sababu kuu zinazofanya watu wafe mapema ni kukosa furaha ya maisha, na kua na afya ambayo sio nzuri.watu wanaoshiriki tendo la ndoa wanapata faida za kua na afya bora na furaha.

Huongeza nguvu za kiume na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa; watu wengi wenye umri zaidi ya miaka 40 huanza kupungukiwa nguvu za kiume. hii ni sababu ya damu kidogo ambayo inafika kwenye uume. tendo la ndoa mara kwa mara hupeleka damu nyingi kwenye uume na kukufanya ue na uume imara na wenye nguvu.

Hukufanya uonekane mdogo kiumri; tendo la ndoa mara kwa mara hukufanya mwili uwe bize kumwaga homoni mbalimbali mwilini ambazo humfanya mtu aonekane mdogo kwa miaka kumi ukilinganisha na umri wake halisi.

Huimarisha afya ya moyo; tendo la ndoa huchoma mafuta ambayo ni sumu kwa moyo, mafuta mengi huweza kuziba mishipa ya moyo na kusababisha shambulio la moyo kitaalamu kama heart attack.

Huongeza nguvu ya misuli ya nyonga; katika umri fulani mkubwa wanawake hupata matatizo ya kushindwa kuzuia mkojo sababu ya kuzaa mara kwa mara. kipindi cha tendo la ndoa wakati mwanamke anafika kileleni uke wake unabana sana na kufanya misuli yake ya nyonga kua na nguvu.

Hupunguza maumivu; utafiti uliofanywa na madaktari bingwa wa mifupa umegundua kwamba wagonjwa wa baridi yabisi au athritis ambao wanashiriki tendo la ndoa mara kwa mara hawasumbuliwi sana na maumivu kama hao wasio shiriki.

Mwisho, wanawake wengi sana walioko kwenye mahusiano au waliolewa hua ni wanakua na sababu nyingi sana za kutoshiriki tendo la ndoa. hii ni moja ya vyanzo vikuu vya wanaume kutoka nje ya ndoa kwani kitaalamu mwanume muda wote ana hamu ya kushiriki tendo la ndoa sasa unapo muwekea vikwazo basi kwenda nje ni lazima.sasa kabla hujaweka vikwazo basi kumbuka faida hizi.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.


Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa



Read More
      edit

Wednesday, May 24, 2017

Published 5/24/2017 01:46:00 PM by

JINSI YA KUANZISHA BIASHARA


Mara nyingi mtu anapotaka kuanzisha biashara anakuwa mwenye kujiamini kwa kuwa atafanikiwa bila kufanya utafiti wa kutosha kwa kuangalia vitu vidogo vidogo vinavyoweza kukwamisha biashara hiyo.
Ni lazima kufanya utafiti wa mahitaji yote yanayohitajika katika biashara hiyo ili kuepuka kufanya vibaya katika biashara yako pamoja na kuandika mpango mkakati wako kufanya hivyo utakuwa umepiga hatua ya kufanikiwa kufikia malengo uliyojiwekea.
Usijifunge kwa shughuli nyingine unazoweza kuwapa wengine wakazifanya, fanya vile tu unavyoweza kufanya, kama una kazi zake mwenyewe ama una wafanya kazi wachache weka utaratibu mzuri wa kiutawala utafanikiwa.Pamoja na hayo pia unapaswa kuwapa wateja wako kile wanachokihitaji, unatakiwa kuuza bidhaa kwa wakati uliopo, si busara kuuza bidhaa yoyote ile bila kuangalia mfumo uliopo wa utandawazi.
Inabidi uwape wateje wako kile wanachokihitaji, unatakiwa uwe na sababu za kuwafanya wateja wako wanunue bidhaa zako kuwashinda washindani wako. Wewe ni mtumishi na wateja wako ni mabosi, Biashara yako ipo kwa ajili ya kuwahudumia wateja na sio wateja kuihudumia. Kama mtumishi anapaswa kufanya kama wateja wake wanavyotaka ili uje kufanikiwa kibiashara.
Mpangilio mbaya hama kutokuwa na mpngilio kabisa hali hii ufanya biashara ndani ya muda mfupi kutokusonga mbele.Biashara unayoifanya unayoifanya isiusike na familia yako kufanya hivyo ni kuiangamiza.
Endapo mwanafamilia anahitaji kitu kutoka kwenye biashara yako inambidi anunue sio kuchukua bure, kwani ili biashara isonge mbele inakubidi uwe mvumilivu.Kawaida biashara yoyote aiwezi kukua kwa siku moja, kwani unatakiwa uwe imara katika malengo uliyojiwekea katika kipindi kigumu unachokipitia.Biashara nzuri ni kama miti mizuri inayochukua muda kukua.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.


Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa


BY Tatu Kiondo
Read More
      edit
Published 5/24/2017 11:46:00 AM by

MAGAZETI YA LEO MAY 24, 2017










Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Read More
      edit

Tuesday, May 23, 2017

Published 5/23/2017 02:13:00 PM by

NGUZO KUU ZINAZOMJENGA MWANAUME KATIKA MAHUSIANO



Kama kichwa kinavyojieleza hapo, siku hizi watu wamejikuta wakichanganyikiwa kutokana na mabadiliko ya kimila na kiutamaduni.
Zamani mtu ulikuwa ukifanya au ukiwa na tabia fulani basi utasikia wazazi wakikuambia hiyo sio tabia ya kike au ya kiume.

Duniani kila jambo huwa na sifa zake halikadhalika tabia.

Naomba wakina Mama ambao wanawatoto wakiume wachukue wajibu wa kuwafundisha watoto tabia zao na sifa zao.
Nguzo zinazomjenga Mwanaume halis

1. Ujasiri 
Mwanaume halisi hawezi kuwa muoga kwani hulka ya mwanaume. Mwanaume sharti Awe jasiri ili aweze kuziba pengo la uwoga wa mwanamke kwani kihulka mwanamke ni muoga ukilinganisha na mwanaume.

2. Busara na hekima.
Mwanaume hapaswi kutoa maamuzi ya kukurupuka wala kutoa hukumu isiyo na haki. Mwanaume halisi huwa na Busara na Hekima katika maamuzi na mazungumzo.

3. Msimamo.
Mwanaume hapaswi kuyumbishwa hata Kama kakosea. Siku zote mwanaume hupaswa kuamini kuwa kile anachokifanya ni sahihi. Hivyo asifanye mambo kwa mashaka mashaka.
Pia aamini kuwa Mwanaume hakosei.

4. Akili na maarifa.
Mwanaume alipewa Tunu zote na Mungu, ili aweze kumfanya awe mfano wake. Mwanaume hupaswa kutenda kwa akili pasipo mihemko yoyote. 
Mwanaume huongozwa na Akili na si kuongozwa na Moyo. Wanaume wengi walioanguka katika ulimwengu huu waliacha kutumia akili ambayo ni miongoni mwa nguzo za mwanaume kamili.

5. Sauti ya Mamlaka
Mwanaume lazima awe na sauti ya kuumba jambo likawa. Akisema kitu kifanyike hufanyika na kinyume chake. Mwanaume hakupewa sauti nzito Kama urembo bali Kama nyenzo ya kutiisha na kuleta utisho.
Mwanaume anapobana sauti ifanane na sauti ya mwanamke huharibu sauti ya mamlaka ambayo humfanya aheshimike.
Mwanaume hapaswa kuongea kwa kujiamini kwa kile anachoongea. Hapaswi kuiga tabia za kishoga au kuelezea habari za kusikia.

6. Mjongeo na Mikao.
Mwanaume hupaswa kutembea kwa mwendo wa kujiamini, mamlaka, kujitukuza. Mwanaume hapaswi kutembea akijitingisha sehemu zake zenye ashki Kama kiuno na makalioni. Jambo hili hufanywa na wanawake.

Mwanaume hapaswi kukaa mikao ya kiumbea, hupaswa kukaa mikao ya ufahari na kujiamini. Sio kujibinua binua.

7. Ubishi.
Mwanaume lazima usikubali kushindwa. Ndio maana unapaswa kuwa na akili. Mwanaume lazima ujue kutetea kile unachokiamini na sio unabisha bila hoja.
Wanaume wasio wabishi huishia kunyanyaswa na wanaume wenzao kwa kupigwa au hata wake zao.
Mwanaume hapaswi kukubali kushindwa kwa lolote na hata Kama anaona atashindwa hapaswi kusema mbele za watu. 
Hii huhusu hata suala la kutafuta maisha.

8. Mwanasanaa.
Mwanaume kamili lazima awe msanii. Kufanya drama kwa mwanaume ni nyenzo muhimi Sana, ucheshi, kuimba, uchoraji n.k. kwaajili ya kumfurahisha yule umpendae.
Mwanaume asipokuwa Msanii huweza kuachwa na mke wake hata Kama ni tajiri wakutupa.
Wanawake hupenda wanaume Wasanii yaani waimbaji, ma-king Drama, waongeaji kwa maneno ya mvuto, wacheshi n.k.
Jambo hili ni tofauti na kinadada hawajajaliwa sanaa Kama wanaume.

9. Kufanya mapenzi.
Mwanaume kamili lazima ajue iwe kwa kujifunza au laa kufanya Mapenzi.
Endapo hutaweza jambo hilo basi utakuwa umepungukiwa pakubwa Sana.
Wanawake huchukulia hicho Kama miongoni mwa vipimo vyao kukupima.

10. Kiongozi.
Sifa zote hapo juu humfanya mwanaume kuwa kiongozi kwa kuiongoza familia na dunia kwa ujumla.


Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa



Read More
      edit