Mara
nyingi mtu anapotaka kuanzisha biashara anakuwa mwenye kujiamini kwa kuwa
atafanikiwa bila kufanya utafiti wa kutosha kwa kuangalia vitu vidogo vidogo
vinavyoweza kukwamisha biashara hiyo.
Ni lazima
kufanya utafiti wa mahitaji yote yanayohitajika katika biashara hiyo ili
kuepuka kufanya vibaya katika biashara yako pamoja na kuandika mpango mkakati
wako kufanya hivyo utakuwa umepiga hatua ya kufanikiwa kufikia malengo
uliyojiwekea.
Usijifunge kwa shughuli nyingine
unazoweza kuwapa wengine wakazifanya, fanya vile tu unavyoweza kufanya, kama
una kazi zake mwenyewe ama una wafanya kazi wachache weka utaratibu mzuri wa
kiutawala utafanikiwa.Pamoja na hayo pia unapaswa kuwapa wateja wako kile
wanachokihitaji, unatakiwa kuuza bidhaa kwa wakati uliopo, si busara kuuza
bidhaa yoyote ile bila kuangalia mfumo uliopo wa utandawazi.
Inabidi uwape wateje wako kile
wanachokihitaji, unatakiwa uwe na sababu za kuwafanya wateja wako wanunue
bidhaa zako kuwashinda washindani wako. Wewe ni mtumishi na wateja wako ni
mabosi, Biashara yako ipo kwa ajili ya kuwahudumia wateja na sio wateja
kuihudumia. Kama mtumishi anapaswa kufanya kama wateja wake wanavyotaka ili uje
kufanikiwa kibiashara.
Mpangilio mbaya hama kutokuwa na
mpngilio kabisa hali hii ufanya biashara ndani ya muda mfupi kutokusonga mbele.Biashara
unayoifanya unayoifanya isiusike na familia yako kufanya hivyo ni kuiangamiza.
Endapo mwanafamilia anahitaji kitu kutoka
kwenye biashara yako inambidi anunue sio kuchukua bure, kwani ili biashara
isonge mbele inakubidi uwe mvumilivu.Kawaida biashara yoyote aiwezi kukua kwa
siku moja, kwani unatakiwa uwe imara katika malengo uliyojiwekea katika kipindi
kigumu unachokipitia.Biashara nzuri ni kama miti mizuri inayochukua muda kukua.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
BY Tatu Kiondo