Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala
maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi
kuwapoteza waume zao. Kilio chao kikubwa ni kukimbiwa na wanaume au
kuachwa.
Leo anakuwa na mwanaume huyu, baada ya muda mfupi kunatokea chokochoko, mwanaume anatimka zake.
Jamaa anamkimbia na kwenda kuanzisha uhusiano mwingine.
Baada ya kukimbiwa, mwanamke hakati tamaa. Anaanzisha uhusiano mwingine,
ndani ya muda mfupi tu, anaambulia maumivu tena. Anabaki kujilaumu.
Hajui chanzo cha yeye
kukimbiwa.
kukimbiwa.
Matokeo ya hili, mwanamke anapoteza uelekeo. Kila mwanaume
anayekutana naye anamkimbia. Mwisho wa siku anajikuta umri umeenda.
Kuolewa inakuwa ni ndoto. Anaanza kulazimisha kusaka mtoto ili angalau
na yeye aitwe mama.
Wanaume wengi hujikuta wakiwaacha wapenzi wao kwa sababu ya
tabia fulani ambazo wakati mwingine huanza taratibu na baadaye huwa
kikwazo kikubwa.
Ili kuweza kuepukana na tatizo hili ni vyema tukaangalia
vitu ambavyo wanaume wamekuwa hawavipendi kutoka kwa wanawake ili kuweza
kujua nini cha kufanya kuhakikisha unamweka mwanaume karibu, asikuache.
1. Chokochoko/Maneno Maneno
Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.

Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa
kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani.
Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi
wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.
Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa
kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo
wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane
na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe
na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.
2. Kutoridhika
Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake, haridhiki tu.
Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao. Anamfanya kila anapokutana naye awaze atapigwa mzinga.

Bahati mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani
kikubwa zaidi. Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi
kuwa na mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume
wengi wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.
Kwake kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake
mbinu za kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika
kwamba wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa
kwake hamtimizii.
Mwanaume akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe
haridhiki, hatoi shukurani ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake.
Taratibu anaanza kujitoa na hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine
ambaye atakuwa anaridhika kwa kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.
3. Kulinganisha
Hii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’
Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa tatizo kubwa.

Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake
kumtamani mtu mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume
mwingine ni nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza
kushawishika kumfuata yule anayemvutia.
Wanawake wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama
umeona kuna kitu kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe
usije kumwambia mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume
uliyenaye ndiye bora kuliko wanaume wote duniani.
4. Kuwa Tegemezi
Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa mwanaume.
Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.

Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya
watoto na mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki
kujishughulisha hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea
familia nyumbani.
Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua
za mwanzoni, ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye
angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata
kwa kutoa wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.
5. Kutokuwa Muelewa
Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.
Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.

6. Kujigamba/Maringo
Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.

Isikupite hii: Mambo matano '5' yatakayo kuongezea thamani katika maisha yako
Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni
vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi
wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume
mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.
7. Kuwa bize sana
Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata akose muda na mwenzi wake.

Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha
unakuwa bize na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume
akose muda wa kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza
kwenda kwa mwanamke mwingine ambaye hayupo bize.
Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza HapaNa.M&U