RUSHA: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan amewaongoza mamia ya waombolezaji waliofika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha na Watanzania wote kuaga miili ya watoto waliofariki kwa ajali ya gari juzi Jumamosi.
Bi Samia Suluhu akitoa salam za pole.
Miili ya marehe ikishushwa kutoka ndani ya gari
Akitoa salam za rambirambi kwa wafiwa na Watanzania wote, Bi Samia amewataka walioguswa na msiba huu kuwa wavumilivu na kumtegemea Mungu hasa katika wakati huu mgumu kwa taifa.
Aidha Bi Samia amemshukuru Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na wananchi wa Tanzania katika msiba uliotokea.
Mzazi akilia kwa uchungu
Miili ya marehemu hao ikiwa tayari kwa kuagwa