Sunday, May 14, 2017

Published 5/14/2017 06:18:00 PM by

MAISHA NI HATUA

Umezaliwa ushinde na utashinda kama utaamini ukweli huo. Wasiwasi unasababisha hofu na ndio chanzo kikuu cha kushindwa, kama una wasiwasi juu ya yatakayotokea kesho, mwezi ujao au mwaka ujao, unajiweka katika hali ya kushindwa katika mafanikio yako kwa kuvuluga mawazo mazuri uliyojipangia.
Kamwe usifikiri kuhusu matatizo ya kwesho, ishi siku ya leo kwa kufanya mipango mizuri uliyoipanga.Na siku zote uwezi kufanikiwa kama unakaribisha wasiwasi au hofu katika maisha yako.

Kama una wasiwasi wa ratiba yako uliyoipanga kwa siku zijazo ni kupoteza nguvu zako, shughulika na mambo yale ambayo ni ya muhimu. Fanya kitu kimoja kwa wakati, usichanganye mambo kwa wakati mmoja. Pia ukiruhusu wasiwasi unakaribisha umaskini katika maisha yako, unatakiwa ukukubaliana na changamoto unazokutana nazo bila kuziogopa.
Fikiria matarajio uliyoyapanga na kuyapa kipaumbele katika akili yako.Kuwa jasiri katika kila hatua unayopitia, ni vema kuzungumzia mafanikio  kwa kila jambo unalolifanya sasa, ni vema kuchangamkia mafanikio.Usiwaze yaliyopita au kushawishika, na kama unasubili mafanikio yakufuate unakosea sasa.
Yawezekana kuwa na amani katika moyo wako, anza sasa kuwa nayo ndani ya moyo wako , usimuamini mtu katika biasha au jambo ulinalolifanya. Kaa ukijua siku zote umezaliwa ushinde na utashinda kama utaamini ukweli huo.


BKwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza HapaNa.M&U
 BY. Tatu Kiondo
      edit