Sunday, May 14, 2017

Published 5/14/2017 02:04:00 PM by

MSICHANA AZUA GUMZO AAMUA KUJIOA MWENYEWE BAADA YA KUKOSA MCHUMBA

Q May Chen Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa.
Mwanamke mmoja ambaye anaugua saratani ya matiti amejioa mwenyewe baada ya kusubiri mchumba kwa muda mrefu.
May Chen mwenye umri wa miaka 28 kutoka Taiwan ameambia BBC kwamba anaugua ugonjwa huo lakini hajakubali sababu hiyo kuhujumu ndoto yake ya kuolewa.
''Nimekuwa nikisubiri mtu kujitokeza na kusema kwamba angependa kufunga ndoa nami mbali na kupiga picha za harusi nami aliambia BBC .


Anasema kwamba wakati unapohisi kwamba huna miaka mingi ya kuishi huna budi kujifanyia maswala ambayo yamekuwa ndoto yako.
Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa.Q May Chen mwanamke mwenye saratni ya matiti aliyejioa
Anasema kuwa wapiga picha walimshauri kupiga picha katika studio lakini yeye akawaambia kwamba anataka picha sawa na zile za harusi.




Hivyobasi alikodisha gari na kwenda kupiga picha hizo katika maandhari ya harusi.
''Nilipovalia rinda la harusi nilijawa na hisia mpaka nikahisi kulia''.
Anasema kwamba alihisi kana kwamba ameafikia ndoto yake ya miaka mingi.
Kwa sababu yeye huugua saratani ya matiti hulazimika kwenda hospitali mara tatu kwa wiki ili kudungwa sindano mbali na kutibiwa kwa kutumia kemikali.
Anaongezea kwamba kwa muda mrefu hakuweza kusimama kwa miguu miwili na kuvaa suruali ndefu, ''nilikuwa nikitembea kwa kiti cha magurudumo''.
Anasema kwamba hakuweza kutembea na kwamba nywele alizo nazo sio nywele zake asilia.



Habari ya mwanamke huo imewagusa watu wengi ulimwenguni.
Q May Chen mwanamke mwenye saratani ya matiti aliyejioa
Anasema kwamba anatumia habari yake kuwapa moyo wanaougua kwamba maisha sio mabaya sana.
''Mbali na maisha na kifo mambo mengine yote ni madogo''.
Anasema kwamba watu wengi wanaougua huwa na wasiwasi wataishi kwa muda gani na lini watafariki ama iwapo matibabu wanayopata yanafanya kazi.
 ''Lakini mimi nawashauri kwamba usiwe na wasiwasi kwa sababu hujui, kwa hivyo kwa nini usijiliwaze''?


Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na 0679979785.


Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza HapaNa.M&U


CHANZO: BBC

      edit